Hoja ya kumuondoa gavana Charity Ngilu yawasilishwa kwa spika

Charity Ngilu
Charity Ngilu
Hoja ya kumuondoa gavana wa Kitui Charity Ngilu ofisini imewakilishwa kwa spika wa bunge la Kitui, Ngilu ameedaiwa kutuma mamlaka vibaya, kukiuka katiba na kutokuwa na nidhamu.

Ripoti znasema hoja hiyo iliwakilishwa na msimamizi wa wadi ya Athi Peter Kilonzo.

“Members of the public are hereby notified that a notice of motion on the impeachment of Kitui Governor Charity Ngilu has been served to the Speaker of the County Assembly." Ripoti zilisoma.

Ripoti hiyo iliuliza wanachama wa umma kutoa maoni yao kuhusu memoranda ambayo iliwasilishwa kwa spika wa kaunti ya Kitui ,wwanachama hao pia walielekezwa maswali au memoranda hiyo iweze kumfikia spika kabla ya tarehe 26,juni Ijumaa mwaka huu.

Wawakilishi wadi kau ti ya Kitui wamejiandaa kuwa na mjadala dhidi ya kumuondoa gavana Ngilu ofisini jumatatu wiki ijayo.