Hakipo tena marudio tu: Kipindi cha Auntie Boss chakamilika

16305_527460090720573_5092456132878709322_n
16305_527460090720573_5092456132878709322_n
Mashabiki wa kipindi cha Auntie Boss watakuwa mbioni kutafuta kipindi chenye ucheshi hii ni baada ya kipindi hicho kutangaza ya kwamba watapeperusha uigizaji wa mwisho wa kipindi hicho mnamo Septemba,16 mwaka huu.

Kipindi hicho kimekuwa kikipeperushwa kwenye runinga ya ntv na marudio kwenye runinga ya maisha magic east, kwa muda wa miaka nane.

Uzalishaji wa kipindi hicho Moonbeam production ilitangaza habari hizo kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya instagram huku wakipakia video yenye muhemko kwenye ukurasa wao.

https://www.instagram.com/p/CFL8SPhimNm/

Kipindi hicho kina misimu 22 na sinema au ukipenda 'episodes' zaidi ya mia moja timu ya uzalishaji iliwashukuru mashabiki kwa kutazama kipindi hicho na hata kuwaunga mkono mika hizo nane.

Kupitia kwenye ukurasa wao wa facebook walikuwa na haya ya kunakili.

"Imekuwa miaka 8 yenye fanaka, misimu,22 na sinema zaii ya mia moja shukrani kwa wote walitazama kipindi siku za wiki kwenye runinga ya ntv

Asanteni kwa kusaidia kipindi hiki tangu mwanzo hadi mwisho, tuna wapenda na kuwashukuru nyote."