Afisa wa polisi aliyeshambulia wakili atazuiliwa hadi tarehe 10 Novemba

Nancy Njeri
Nancy Njeri
Image: courtesy

Afisa wa  polisi Nancy Njeri anazuiliwa hadi Novemba 10 wakati kesi  ya mauaji dhidi yake itaendelea kumruhusu afanyiwe uchunguzi wa Covid na akili.

Njeri anatuhumiwa kwa mauaji ya wakili Onesmus Masaku wiki mbili zilizopita kwa kukata mikono yake.

Wakili huyo atazikwa hapo kesho.

ZiIfuatazo ni mkusanyiko wa habari mbalimbali humu nchini,

Mbunge wa  malindi Aisha Jumwa ataendelea kuzuiliwa na polisi baada ya kukosa shillingi millioni nne ya kuwachiliwa kwa dhamana.Jumwa na masaidizi wake Geoffrey Otieno waliachilia hapo jana kwa dhamana na wakaamuriwa  kuwasilisha stakabadhi zao za kusafiri mahakamani.

Zaidi ya wafungwa 1,700 wameambukizwa virusi vya corona .Dkt Azenga Kisivuli anasema wafungwa watatu wamefariki kutokana na virusi hivyo. Kamishna mkuu wa idara ya magereza Wycliffe Ogalo amesema ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona katika magereza linatokana na ugumu wa kuzingatia kanuni ya mtu kukaa umbali wa mita moja kutoka kwa mwenzake.

Shule za kibinafsi zimesitisha shughuli za kufunguliwa kwa shule kwa mara ya  pili ambayo ilitarajiwa tarehe 26 Oktoba. Muungano wa shule hizo unasema uamuzi huo ni kutokana na kuongezeka kwa virusi vya covid 19 humu nchini. Hata hivyo wanasema kwamba wanafunzi walio shuleni kwa sasa wataendelea na masomo yao.

Tunapokaribia mwisho wa uhamasisho kuhusu saratani ya matiti  Daktari  Geofry Mutuma anashauri wanawake wenye umri chini ya miaka 35 kujifanyia uchunguzi wa saratani ya matiti kwa kuyatomasa na walio na zaidi ya umri huo kufanyiwa na njia ya kiteknolojia, Mamogramu. Daktari Mutuma anasema hii ndio njia bora ya uchunguzi .

Rais Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa wakaazi wa Nairobi kumuunga mkono mkurugenzi wa NMS Mohammed Badi katika azma yake ya kubadilisha miundombinu ya kaunti hiyo. Wakati huo huo amemkosoa Gavana Mike Sonko akisema hakuna mtu anayetaka kumshambulia au kunyakua mamlaka yake.