Moses Kuria aomba radhi kwa kusema Sonko ni Kinara wa Wakamba

Muhtasari
  • Moses Kuria aliozomewa sana na viongozi wa Ukambani
  • Kuria alisema kwamba Sonko anapaswa kuwa kiongozi wa Ukambani.
  • Moses Kuria alisema kwamba kosa lake lilikuwa kutoa maoni hayo 
FILE_1575031167__1577790071_92124
FILE_1575031167__1577790071_92124

Mbunge wa Gatundu Moses Kuria amezungumza na kulazimika kuomba msamaha kutokana na usemi wake kuwa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko anapaswa kuwa kiongozi wa ukambani.

Meneo ya Kuria hayakuchuliwa vyema na baadhi ya viongozi wakati wa mazishi ya seneta wa Machakos Boniface Kabaka.

Kupitia ukurasa wake wa facebook, Kuria alidai kwamba kosa lake lilikuwa  ni kutoa maoni yake kwamba Sonko anapaswa kuwaongoza wananchi wa jamii ya Ukambani na kutoa mustakabli wa siasa zao.

 

Alisisitiza kuwa Sonko amechaguliwa vyema na watu wa jamii zingine na ushawishi mkubwa nje ya ukambani kuliko kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka.

Mbunge huyo aliomba msamaha na kusema kuwa ameridhia usemi wake siku ya Jumanne.

"Oh ye wanafiki. Jana nilikuwa chanzo cha chuki na kushambuliwa vikali na seneta wa kaunti ya Kitui Enock Mutua

Nilitoa maoni yangu kuwa Sonko  anapaswa kuwa kiongozi wa Ukambani, kwa uchungu mbunge Makali Mulu, seneta Wambua, Cleophas Malala, Moses Wetangula na Mutula Kilonzo Jr ambao walisema kwamba ningesema hayo nikiwa sehemu ya Nyanza ningerudi kwangu nyumbani bila shati.

Nachukua fursa hii kuomba msamaha kwa chivu Kivoi wa ukambani." Ilisoma sehemu moja ya ujumbe wa Kuria.

(MHARIRI: DAVIS OJIAMBO).