Msimuamini Uhuru,'Boni Khalwale aonya jamii ya Luhya baada ya usemi wake rais

Muhtasari
  • Boni Khalwale aonya jamii ya waluhya baada ya usemi wake Uhuru Kenyatta kuhusu utawala wa nchi
  • Mwanasiasa huyo aliambia jamii hiyo haipaswi  kuamini use i wake Uhuru
khalwale
khalwale

Aliyekuwa seneta wa kaunti ya Kakamega Boni Khalwale kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook ameonya jamii ya luhya dhidi ya kumuamini rais Uhuru Kenyatta.

Hii ni baada ya matamshi yake rais siku ya jumamosi wakati wa mazishi yake mama Hannah Mudavadi aliposema kwamba ni wakati wa kabila nyingine kuchukua utawala wa nchi ya kenya.

Kulingana na Khalwale ambaye ni mfuasi sugu wa naibu rais William Ruto njia moja ya waluhya kujipata mamlakani ni kujiunga na timu ambayo itashinda katika uchaguzi.

 
 

Pia aliwaonya waluhya dhidi ya kumuamini rais kwa ajili ya matamshi yake.

Huu haoa ujumbe wake Khalwale;

"Watu wauei wa Maragoli hamna kitu kipya ambacho rais alisema katika usemi wake, hamna mtu ambaye atatuzawadi urais kwa maana khuli Bauhyia

Mahali pa kuanza ni pala Kijana Wamalwa alituachia, yaani tuweze kujiunga na timu ambayo imebeba ushindi

Msimuamini rais Uhuru Kenyatta, kwa mara nyingine anacheza na akili zetu, anaweza kusema hayo akiwa magharibi lakini si nyumbani kwake." Aliandika Boni.

Ujumbe wake Khalwale uliibua hisia tofauti huku wanamitandao wakitoa hisia zao kuhusu matamshi ya rais na ujumbe wake Khalwale.