Viongozi wa kidini wataka amani kudumishwa wakati wa kampeni

Unashauriwa kuhudhuria vikao vya umma na vile vile utenge muda wa kusoma na kuelewa mswada wa BBI ili kufanya  uamuzi wa busara wakati wa kura ya maoni.

Viongozi wa kidini wa eneo la North Rift wakiongozwa na Joseph Oketch pia amemtaka Rais Uhuru Kenyatta kuhakikisha viongozi wanaochochea vita  na ukabila kuchukuliwa hatua za kisheria.

Katika mkusanyiko wa habari za kisiasa ni kuwa;

Naibu Rais William Ruto anasema hatishiwi na miungano yoyote inayobuniwa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022. Ruto alizuru kaunti ya Trans Nzoia  jana na anatarajiwa kuzuru kaunti ya Murangá hii leo.

Rais Uhuru  Kenyatta amechaguliwa kama mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Uhuru anachukua usukani kutoka kwa mwenzake Rais wa Rwanda Paul Kagame. Daktari Peter Mathuki kutoka Kenya ameteuliwa kuwa katibu mkuu mpya wa Jumuiya kwa muda wa miaka mitano .

Kinara wa ODM Raila Odinga hii leo atakuwa akizuru kaunti ya Busia na anatarajiwa kuanza ziara yake kwa kuhudhuria misa katika kanisa katoliki la Lwanya mwendo was aa nne. Wakati huo huo Seneta Irungu Kangáta atakuwa mwenyeji wa naibu rais William Ruto katika eneo la Gatanga kaunti ya Murangá.