Wapelelezi wabaini kuwa Jennifer Wambua hakutekwa nyara

Jennifer Wambua
Jennifer Wambua
Image: HISANI

Wapelelezi wanaouchunguza mauaji ya aliyekuwa naibu mkurugenzi wa mawasiiano katika tume ya ardhi nchini Jennifer Wambua, wanasema hakutekwa nyara kabla ya kutoweka kwake.

Inaaminika kuwa Wambua alipanda matatu kuelekea Ngong, baada ya kushauriwa na mhubiri mmoja aliyemtaka kwenda kufanyiwa maombi ili apate kupona msongo wa mawazo. Polisi wanamzuilia mwanamume anayedaiwa kumpa maji ya kunywa kabla ya kumnajisi na kisha kumnyonga.

Ufuatao ni mkusanyiko wa habari humu nchini:

Waandishi tisa wa habari na mbunge mmoja wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Matuu, baada ya kupatikana katika purukushani la kuwafurusha watu kutoka kwa ardhi inayokumbwa na mzozo, katika kijiji cha Makima huko Mbeere Kusini kaunti ya Embu.

Zaidi ya familia elfu 5 zimewachwa bila makao zikikadiria hasara na kusema kuwa hawakupewa ilani ya kuondoka.

Rais Uhuru Kenyatta anazitaka taasisi za usalama kuwapa kipa umbele wahitimu wa NYS katika fursa za ajira. Rais alisema haya wakati wa hafla ya kufuzu kwa NYS huko Gilgil jana ambapo makurutu elfu 7 walifuzu. Rais aliwapongeza makurutu hao kwa jukumu walilolitekeleza la kuboresha nchi hii na wanapoendelea kufanya hivyo wakati huu wa janga la corona.

Wanaume wametakiwa kubadili dhana kwamba wanawake ambao wamewezeshwa hawawezi kuwa wake wazuri na badala yake wajitahidi kujiboresha ili wafikie kiwango chao.

Mshauri wa familia James Mbugua anasema haifai kudhania kuwa wanawake waliowezeshwa wanapaswa kuwa na tabia sawa na ambao hawajawezeshwa, na kuwa hakuna makosa kwa wanawake kuvunja kanuni za kijamii.

Ifanye kuwa tabia ya kumsomea mwanao vitabu kuanzia umri mdogo kwani itamsaidia kujua maneno mapya na pia kuboresha uwezo wao wa kuwa makini. Mtaalamu wa usemi Lorna Ochido anasema pia itawapa utamaduni wa kusoma na kuwafanya wajue mambo mengi.