Hapo sasa! Raila asheherekea baada ya seneti na bunge kupitisha muswada wa BBI

Muhtasari
  • Raila asheherekea baada ya seneti na bunge kupitisha muswada wa BBI

Kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) Raila Odinga anafyraha baada ya bunge la seneti kupitisha Initiative Bridges Initiative (BBI).

Seneti na bunge la kitaifa walipiga kura na kupitisha muswada wa BBI.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter kigogo huyo alisema kwamba mpira unapaswa kusonga mbele huku akiwashukuru maseneta.

Maseneta 51 walipiga kura na kupitisha muswada huo huku 11 wakipiga kura ya la.

"Hapo sasa!Vizuri sana kwa @Senate_KE and @NAssemblyKE kwa kupitisha muswada wa BBI 

#Ball Mbele!," Aliandika Raila.