Rafikiye mfanyabiashara wa Eastleigh alifanikisha utekaji nyara; Mshukiwa alikamatwa katika chumba cha wageni Naivasha

Uchunguzi wa polisi ulibaini kuwa washukiwa walikuwa wametoa Sh650,000 kutoka kwa akaunti ya benki ya Lukman wakati alikuwa ametekwa nyara.

Muhtasari

•Polisi walisema kuwa Hafsa na Njogu walifuatiliwa hadi kwenye hoteli moja mjini Naivasha ambako walikuwa wamejificha tangu Lukman anusuriwe kutoka ndani ya tenki la maji kwenye nyumba moja maeneo ya Matopeni, Kayole.

•Polisi wamefichua kuwa waliomteka nyara Lukman walimdanganya na dili ya kusambaza tikiti maji kisha kudai kulipwa milioni 5.

Hafsa Mohamed Abdi, Lukman na Njogu
Hafsa Mohamed Abdi, Lukman na Njogu

Mwanamke aliyekuwa anadhaniwa kuwa ametekwa nyara jijini Nairobi wiki mbili zilizopita alipatikana katika hoteli moja ya wageni mjini Naivasha siku ya Jumapili.

Maafisa wa polisi walidai kuwa alikuwa mmoja wa waliopanga njama ya kuteka nyara rafiki yake  mwanabiashara, Hafsa Mohamed Lukman, 23, aliyetoweka mnamo Juni 15.

Hafsa Ahmed Abdi alipatikana pamoja na mshukiwa aliyekuwa anatafutwa kufuatia utekaji nyara huo.

Mshukiwa, Jackson Njogu ni mwanabiashara upande wa Kayole ambako Lukman alitekwa nyara.

Polisi walisema kuwa Hafsa na Njogu walifuatiliwa hadi kwenye hoteli moja mjini Naivasha ambako walikuwa wamejificha tangu Lukman anusuriwe kutoka ndani ya tenki la maji kwenye nyumba moja maeneo ya Matopeni, Kayole.

Ilisemekana kuwa wawili hao walidai kulipwa milioni 5  baada ya kumteka nyara Lukman. Hata hivyo, mhasiriwa aliokolewa tarehe Juni 20.

Uchunguzi wa polisi ulibaini kuwa washukiwa walikuwa wametoa Sh650,000 kutoka kwa akaunti ya benki ya Lukman wakati alikuwa ametekwa nyara.

Baada ya kupata pesa hizo, wawili hao walitoweka kuelekea Kinangop ambako walinunua baa ambayo wamekuwa wakifanyia biashara.

Kufikia sasa washukiwa watatu wametiwa mbaroni kuhusiana na kesi ya Lukman.

Polisi wamefichua kuwa waliomteka nyara Lukman walimdanganya na dili ya kusambaza tikiti maji kisha kudai kulipwa milioni 5.

Hafsa amekuwa akifanya biashara ya kuuza tikiti maji ambazo anapata kutoka Bura, Garissa.

Konstabo Mary Wandia wa kituo cha polisi cha Buruburu aliarifu mahakama kuwa mnamo Juni 22, mshukiwa kwa jina Syrus Ndung'u Njogu alimpigia simu Lukman na kumuagiza wapatane maeneo ya Kayole junction ili aingizwe kwenye biashara ya kuuza tikiti maji.

Alipofika Kayole Junction akiambatana na Hafsa, waliingia ndani ya duka moja na kuswali. Walikuwa wanatoka nje, walikabiliwa na wanaume wawili ambao waliwapeleka mahala fiche

Njogu alikamatwa baada ya simu yake kufuatiliwa karibu na mahali Hafsa alikuwa ametekwa nyara. Wandia aliarifu mahakama kuwa Njogu alikuwa akizungumza na washukiwa ambao walikuwa mafichoni.

"Mnamo Juni 20, mhasiriwa aliweza kuona nje kupitia mwanya nakuona mtoto aliyekuwa anapita na kumuomba usaidizi" Konstabo Wandia alisema.

Mtoto yule alimuarifu babake ambaye alipiga ripoti katika kituo cha polisi cha Kayole na Lukman akaokolewa.

Imebainika kuwa Hafsa alikodishwa chumba ambacho Lukman alikuwa amefungiwa ila hakulipa mwanzo. Alilipa siku nne baadae na pesa ambazo alitoa kwa simu ya Lukman.

Baadae watekaji nyara walileta tenki ambalo waliweka Lukman ndani na bidhaa zingine za nyumba.  Majirani wameeleza kuwa muziki uliochezwa kwa nguvu ungesikika mara kwa mara kutoka ndani ya chumba kile.

Polisi wanaendelea kutafuta washukiwa wengine.

(Utafsiri: Samuel Maina)