Jamaa afariki baada ya kutumia Viagra Murang'a

Inaripotiwa kuwa pakiti moja ya viagra ilipatikana ndani ya bafu.

Muhtasari

•Kulingana na ripoti ya polisi, Fredrick Opiyo (50) alifariki akiwa ndani ya chumba cha malazi cha hoteli iliyo maeneo ya Murang'a  baada ya kutoka kwenye bafu anakodaiwa kutumia dawa hizo.

•Mwende alipokuwa ndani ya bafu aliskia Opiyo akigumia, akatoka haraka na kumpata bila nguo huku akiwa amekumbwa na matatizo ya kupumua. Hapo ndipo alijulisha mlinzi wa hoteli hiyo.

crime scene 1
crime scene 1

Mwanaume mmoja  anaripotiwa kufariki Jumanne  usiku baada ya kutumia Viagra katika hoteli moja kaunti ya Murang'a usiku wa

Kulingana na ripoti ya polisi, Fredrick Opiyo (50) alifariki akiwa ndani ya chumba cha malazi cha hoteli iliyo maeneo ya Murang'a  baada ya kutoka kwenye bafu anakodaiwa kutumia dawa hizo.

Kwa wakati huo alikuwa na Mary Mwende (35) aliyeungana naye saa moja baada yake kukodishwa chumba hicho.

Wawili hao walifurahia chakula cha jioni pamoja kabla ya Opiyo kuelekea bafuni. Mwende aliingia bafuni pia punde baada yake kutoka na kujilaza.

Mwanamke huyo alipokuwa  pale ndani aliskia Opiyo akigumia kwa uchungu, akatoka haraka na kumpata bila nguo huku akiwa amekumbwa na matatizo ya kupumua. Hapo ndipo alimjulisha mlinzi wa hoteli hiyo.

"Mpira wa kondomu uliokuwa umetumika na mwingine ambao haukuwa umetumika ulipatikana ndani ya chumba hicho" Ripoti ya polisi ilisoma.

Inaripotiwa kuwa pakiti moja ya viagra pia ilipatikana ndani ya bafu.

Polisi wanaendelea kuchunguza kuhusiana na tukio hilo huku mwili wa marehemu ukihifadhiwa katika mochari ya Murang'a Teaching and Referral Hospital.