Jamaa apatikana akinusa chupi za wanawake Ngong, adai kuwa anashuku amerogwa

Jamaa huyo ambaye ana umri wa miaka 35 alinusurika kifo baada ya kuokolewa kutoka mikononi mwa wakazi wa ploti hiyo waliojawa na hasira ambao walitaka kumchoma

Muhtasari

•Kizaazaa kiliibuka katika ploti moja maeneo ya Ngong baada ya jamaa mmoja ambaye ni mhudumu wa bodaboda kupatikana akinusa chupi za wanawake.

•Inadaiwa kuwa baba huyo wa watoto wawili alionekana akitekeleza kitendo hicho cha aibu na mume wa mwanamke aliyekuwa ameanika chupi zake kwenye kamba.

Chupi za wanawake zikiwa zimeanikwa kwa kamba
Chupi za wanawake zikiwa zimeanikwa kwa kamba
Image: HISANI

Habari na Kurgat Marindany

Kizaazaa kiliibuka katika ploti moja maeneo ya Ngong baada ya jamaa mmoja ambaye ni mhudumu wa bodaboda kupatikana akinusa chupi za wanawake.

Jamaa huyo ambaye ana umri wa miaka 35 alinusurika kifo baada ya kuokolewa kutoka mikononi mwa wakazi wa ploti hiyo waliojawa na hasira ambao walitaka kumchoma.

Inadaiwa kuwa baba huyo wa watoto wawili alionekana akitekeleza kitendo hicho cha aibu na mume wa mwanamke aliyekuwa ameanika chupi zake kwenye kamba.

Mumewe mmiliki wa chupi zile alighadhabishwa na kitendo hicho na kushawishi wakazi wengine wachukue hatua mikononi.

Hata hivyo, msimamizi wa ploti aliweza kutuliza hali na  kuokoa maisha ya jamaa huyo ambayo yalikuwa mashakani.

Alipokuwa anahojiwa kuhusiana na tukio hilo, mhusika alisema kwamba anashuku kuwa amerogwa kwani amekuwa akifanya kitendo hicho kwa muda sasa.