Maajabu haya! Wezi waiba viti vya kanisa na vikombe vinavyotumika wakati wa ushirika mtakatifu, Kisii

Kiongozi wa kanisa alisema kwamba sinia na vikombe vya ushirika mtakatifu haziwezi kutumika manyumbani na kuagiza waliochukua kuzirejesha kanisani.

Muhtasari

•Hali ya mshangao iliibuka maeneo ya Bonchari baada ya genge la wezi kuvamia  kanisa la Gesonso SDA na kuiba mali ya kanisa yenye dhamani kubwa isiyojulikana

•Mogusu ametoa ombi kwa maafisa wa polisi kufanya hara katika upelelezi kuhusiana na wizi huo kwani waumini wanatazamia kurejelea ibada zao za kawaida kanisani siku ya Jumamosi kuona kuwa serikali imeruhusu kanisa zilizokuwa zimefungwa maeneo hayo zifunguliwe.

Vikombe vya ushirika mtakatifu
Vikombe vya ushirika mtakatifu
Image: DREAMTIME.COM

Habari na Mercy Osongo

Hali ya mshangao iliibuka maeneo ya Bonchari baada ya genge la wezi kuvamia  kanisa la Gesonso SDA na kuiba mali ya kanisa yenye dhamani kubwa isiyojulikana.

Shemasi Simon Mogusu amesema kuwa washirika wa kanisa hilo walipigwa na butwaa baada ya kufika kanisani na kupata kuwa viti na vyombo vinavyotumika katika ibada  ya ushirika mtakatifu havikuwepo.

"Tulipata kuwa zaidi ya viti 150, sinia na vikombe vinavyotumika wakati wa ushirika mtakatifu havikuwepo pale kanisani" Mogusu alisema.

Kiongozi huyo wa kanisa alisema kwamba sinia na vikombe vya ushirika mtakatifu haviwezi kutumika manyumbani na kuagiza waliochukua kuzirejesha kanisani.

Mogusu ametoa ombi kwa maafisa wa polisi kufanya hara katika upelelezi kuhusiana na wizi huo kwani waumini wanatazamia kurejelea ibada zao za kawaida kanisani siku ya Jumamosi kuona kuwa serikali imeruhusu kanisa zilizokuwa zimefungwa maeneo hayo zifunguliwe.

Kesi hiyo iliripotiwa katika kituo cha polisi cha Gesonso na upelelezi kung'oa nanga.