Polisi ajitoa uhai kwa kujiteketeza akiwa ndani ya nyumba yake Kieni

Mke wa marehemu alikuwa amesafiri kuenda Muranga na watoto wao hawakuwa nyumbani wakati tukio hilo lilitokea siku ya Jumatatu.

Muhtasari

•Inaripotiwa kuwa afisa huyo ambaye amekuwa akifanya kazi maeneo ya Kiambu alikuwa katika likizo ya siku kadhaa tangu mapema mwezi huu.

•Kulingana na polisi, mke wa marehemu alikuwa amesafiri kuenda Muranga na watoto wao hawakuwa nyumbani wakati tukio hilo lilitokea siku ya Jumatatu.

•Inadaiwa kuwa waliofika katika eneo la tukio walipata mlango ukiwa umefungwa upande wa ndani.

crime scene
crime scene

Polisi wanachungunza kisa kimoja ambapo afisa mwenzao kutoka kituo cha Kiambu anadaiwa kujitoa uhai kwa kujiteketeza akiwa nyumbani kwake maeneo ya Kieni Magharibi kaunti ya Nyeri.

Kulingana na polisi, mke wa marehemu alikuwa amesafiri kuenda Muranga na watoto wao hawakuwa nyumbani wakati tukio hilo lilitokea siku ya Jumatatu.

Inaripotiwa kuwa afisa huyo ambaye amekuwa akifanya kazi maeneo ya Kiambu alikuwa katika likizo ya siku kadhaa tangu mapema mwezi huu.

Majirani walijumuika nyumbani kwa afisa huyo baada ya kuona moshi mkubwa usio wa kawaida ukitokea pale na kujitahidi kuzima moto uliokuwa umeanza kuteketeza nyumba ile.

Inadaiwa kuwa waliofika katika eneo la tukio walipata mlango ukiwa umefungwa upande wa ndani.

Baada ya mlango kuvunjwa mwili wa afisa huyo ulipatikana chumbani chake cha malazi na kupelekwa katika mochari moja maeneo hayo huku upelelezi ukiendelea.

Hii ni kesi ya hivi karibuni  ya mtu kujitoa uhai nchini Kenya kuripotiwa huku kesi hizo zikiwa zimekithiri mno.