Makali ya corona:Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 6,597,597

Muhtasari
  • Kenya imesajili visa 35 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 4,246 chini ya saa 24 zilizopita
  • Kati ya maambukizi hayo 33 ni wakenya huku 2 wakiwa raia wa kigeni,22 ni wanaume huku 13 wakiwa wanawake
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,816 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 0.8%
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MAKTABA

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 6,597,597.

Kenya imesajili visa 35 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 4,246 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 33 ni wakenya huku 2 wakiwa raia wa kigeni,22 ni wanaume huku 13 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,816 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 0.8%.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 5 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 79.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,811,260.

Aidha watu 26 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 248,018,22 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 4 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Watu 2 wameaga dunia kutokana na corona huku idadi jumla ya walioaga dunia ikifika 5,332.

Kuna wagonjwa 346 ambao wamelazwa hospitalini, 973 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 20 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).