Uko wapi wakati nakuhitaji,ahadi za bure hazitakupeleka mahali-Rais Uhuru amlipua naibu wake

Muhtasari
  • Mkutano wa mwaka huu ni mkutano wa kwanza wa ana kwa ana tangu Covid-19 ilipoikumba Kenya mnamo 2020

Rais Uhuru Kenyatta na Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli leo wameungana na wafanyikazi kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi katika Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo.

Mkutano wa mwaka huu ni mkutano wa kwanza wa ana kwa ana tangu Covid-19 ilipoikumba Kenya mnamo 2020.

Siku hii imetengwa kwa ajili ya kuenzi na kutambua vyama vya wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi kwa michango yao kwa nchi.

Huku akizungumzia gharama ya juu nchini, rais alimlipua naibu wake kwa kumlaumu na matusi, huku akimuuliza yuko wapi wakati anamhitaji.

Aidha rais Kenyatta alisema kwamba anamshukuru kinara wa ODM Raila Odinga.

PIa aiwashauri wanasiasa kwamba ahadi za bure kwa wakenya hazitawapeleka mahali.

"Mimi sikuwa Ukraine kuanzisha vita, ati unasema vitu vimepanda tumuulize Uhuru, badala uje tusaidiane mnaenda kwa masoko na matusi matusi na ahadi za bure hazitakupeleka mahali

Uko wapi wakati nakuhitaji tusaidiane tufanye kazi, lakini kazi ni matusi Na unajiita kiongozi na pia ati wewe ni namba ngapi katika nchi?... Basi si ungewacha mimi nitafute mtu ambaye angenisaidia? Wewe unajua hii sio shida ya mtu, na mshukuru huyu mzee," Uhuru alizungumza

Waziri wa Leba Simon Chelugui pia alihudhuria sherehe hizo.

Viongozi wengine waliohudhuria sherehe hizo ni Gavana wa Nairobi Anne Kananu, Mwakilishi wa Wanawake wa Nairobi Esther Passaris na katibu mkuu wa ODM ODM Edwin Sifuna.