Waombolezaji wateketeza nyumba Kisii kulipiza kisasi

Umati huo ulikuwa ukirejea nyumbani Alhamisi jioni na mwili wa Boaz Orina.

Muhtasari

•Katika eneo linaloshukiwa kuwa la kuuza chang'aa, walibomoa duka moja na kuchoma nyumba ya familia.

•Mwili wa Orina uligunduliwa ukitapakaa kando ya njia inayoshukiwa kuwa eneo la kuuza Changaa wiki mbili zilizopita.

Eneo linaloshukiwa kuwa la kuuza Changaa katika kijiji cha Nyamesocho akifuka moshi baada ya hafla ya mazishi iliyosababisha ghadhabu kuteketeza Alhamisi jioni.
Eneo linaloshukiwa kuwa la kuuza Changaa katika kijiji cha Nyamesocho akifuka moshi baada ya hafla ya mazishi iliyosababisha ghadhabu kuteketeza Alhamisi jioni.
Image: MAGATI OBEBO

Umati umeteketeza nyumba mbili za makazi katika eneo la Nyamesocho, Masaba Kusini, kaunti ya Kisii kufuatia mauaji ya mtu aliyekuwa akijiburudisha katika eneo hilo wiki mbili zilizopita.

Umati huo ulikuwa ukirejea nyumbani Alhamisi jioni na mwili wa Boaz Orina lakini kabla ya kufika nyumbani, vijana waliokuwa na silaha waliongoza magari hadi eneo la tukio na kubomoa nyumba.

Katika eneo linaloshukiwa kuwa la kuuza chang'aa, walibomoa duka moja na kuchoma nyumba ya familia.

Aidha walibomoa nyumba nyingine inayomilikiwa na mwanakijiji mmoja anayeaminika kuwa mshukiwa mkuu wa mauaji ya marehemu.

Maafisa kutoka Ramasha walitembelea eneo hilo saa chache baada ya uharibifu huo.

Mwili wa Orina uligunduliwa ukitapakaa kando ya njia inayoshukiwa kuwa eneo la kuuza Changaa wiki mbili zilizopita.

Alionekana akifanya sherehe katika eneo la kuuza chang’aa la Nyagentinge ambapo mwili huo ulipatikana.

Thomas Ongoge, mwenyeji alisema nyumba hizo ni za Matara Omwoyo na Nyagentinge Nyansikera.