Jowie Irungu awasilisha ombi la kukata rufaa dhidi ya hukumu ya kifo

Notisi hiyo inaonyesha kuwa jowie anakusudia kupinga hukumu yake kwa mauaji hayo na baadae kuhukumiwa na jaji Grace Nzioka.

Muhtasari
  • Jaji Nzioka alimkabidhi Jowie hukumu kali zaidi kwa mauaji akisema kuwa adhabu hiyo inalingana na uhalifu mbaya uliogharimu maisha ya Monica aliyekuwa na  umri wa miaka 29.
katika Mahakama ya Milimani kabla ya hukumu ya mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani Februari 9, 2024.
Joseph Irungu almaarufu Jowie katika Mahakama ya Milimani kabla ya hukumu ya mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani Februari 9, 2024.
Image: DOUGLAS OKIDDY

Joseph Irungu almaarufu Jowie amewasilisha ombi la kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama kuu iliyomhukumu kifo kwa kosa la mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani 2018.

Notisi hiyo inaonyesha kuwa Jowie anakusudia kupinga hukumu ya kifo baada ya mahakama kumpata na hatia ya kumuua Monica Kimani. 

"Kumbuka kwamba Joseph Kuria Irungu almaarufu Jowie alikata rufaa katika mahakama ya Rufaa kupinga uamuzi wa mheshimiwa jaji Grace Nzioka uliotolewa katika mahakama ya Milimani, Nairobi mnamo tarehe 9 Februari 2024 na katika hukumu yake iliyoandikwa tarehe 9 Februari 2024 ambapo mrufani alipatikana na hatia ya mauaji na kuhukumiwa kifo mnamo Machi 13, 2024. Rufaa hiyo ni kupinga hukumu hiyo", inasoma hati ya mahakama iliyowasilishwa kupitia wakili wake Andrew Muge.

Jaji Nzioka alimkabidhi Jowie hukumu kali zaidi kwa mauaji akisema kuwa adhabu hiyo inalingana na uhalifu mbaya uliogharimu maisha ya Monica aliyekuwa na  umri wa miaka 29.

Jaji alibainisha kuwa kulikuwa na chaguzi tatu pekee katika kumhukumu Irungu ambazo ni pamoja na kifungo cha maisha au kifo.

Hakimu alisema aliegemeza uamuzi wake kutokana na uzito wa ushahidi uliotolewa wakati wa kesi hiyo na pia tabia ya mfungwa.