Wanne waokolewa baada ya 'flyover' ya barabara kuu ya Kangemi kuanguka, uokoaji unaendelea

Muhtasari
  • Wanne waokolewa baada ya kuanguka kwa barabara kuu ya Kangemi, uokoaji unaendelea

Watu wanne wameokolewa baada ya sehemu ya barabara mpya ya Kangemi inayoendelea kujengwa kuanguka juu yao Jumatatu jioni.

Wawili ambao walipata majeraha walikimbizwa hospitalini na wanapata matibabu.

Wengine kadhaa wanahofiwa kunaswa chini ya kifusi, huku bosi wa kaunti ya Westlands Lilian Obura akithibitisha kuwa juhudi za uokoaji zinaendelea.

Idadi ya wale waliohofiwa kunaswa haikujulikana

Mengi yafuata;