Mahakama ya juu kutoa uamuzi kuhusu BBI siku ya Alhamisi

Muhtasari

• Uamuzi kuhusu kesi ya mswada wa BBI kutolewa Alhamisi saa tatu asubuhi.

• Taarifa zaidi kutolewa kuhusu uamuzi huo.

Star, KWA HISANI
Star, KWA HISANI
Image: Martha Koome

Mahakama ya juu [Supreme Court] imesema kwamba itakuwa inatoa rasmia uamuzi wake kuhusu mswada wa BBI Alhamisi, tarehe 31 mwezi Machi.

Katika taarifa, msajili wa mahakama ya juu Letizia Wachira alisema kwamba uamuzi huo utatolewa saa tatu asubuhi.

"Ifahamike kwamba uamuzi kuhusu suala hili utawasilishwa Alhamisi tarehe 31 mwezi Machi mbele ya mahakama ya juu nchini," taarifa hiyo ilisema.

Awali, mahakama ya rufaa na mahakama kuu ziliupiga shoka mswada huo kwa kile kilichotajwa kuwa mchakato huo kukiuka katiba.