Fomu 34A hazikuhitilafiwa kwa njia yoyote - Jaji Martha Koome

Koome alisema hakukuwa na ushahidi wa kutosha kudhibitisha kama kulikuwepo na mapungufu.

Muhtasari

• Alisema hakukuwa na utofauti wowote wa kina kati ya fomu 34A zilizotumwa kwenda IEBC na zile zilisowasilishwa kimwili.

Jaji wa mahakam ya juu Martha Koome
Jaji wa mahakam ya juu Martha Koome
Image: maktaba

Jaji wa mahakama ya upeo Martha Koome amepuuzilia mbali madai yaliyoibuliwa na upande wa malalamishi kwamba fomu 34A zilikuwa na mapungufu wakati wa kusukumwa kutoka vituo vya kupiga kura hadi IEBC.

 Akisoma uamuzi wa jopo la majaji saba wa mahakama hiyo, Koome alisema pia kwamba hata kama ripoti ya ukaguzi wa sajili ya wapiga kura ilitolewa siku 7 tu kelekea uchaguzi mkuu, sajili hiyo ilitumika bila mapungufu yoyote.

Akizungumzia madai ya uwepo wa mtu aliyekuwa katika seva za IEBC, jaji Koome alisema kwamba hakukuwa na ushahidi kwamba kulikuwepo na mtu kama huyo.

Alhamis wakili Julie Soweto aliibua madai kwamba kulikuwepo na mtu katika seva za IEBC kwa jina Jose Carmargo ambaye kulingana na yeye ndiye alibananga matokeo kwa upendeleo wa Ruto.

Vile vile jaji Koome alisema kwamba ushahidi uliowasilishwa na upande wa malalamishi haukuwa na uzito wa kuwafanya waamini kwamba teknolojia ya IEBC ilifeli.

Majaji wa Mahakama ya Juu walikubaliana na Tume Huru ya Mipaka ya Matangazo ya Uchaguzi kwamba mfumo wa IT wa uchaguzi uliotumiwa katika uchaguzi wa 2022 ulikuwa salama.

"Kwa maoni yetu, walalamishi walishindwa kutoa ushahidi kinyume chake," Koome alisema.