Ramaphosa anusurika katika kura za wabunge

Katika kile ambacho kilianza kama kikao chenye mvutano bungeni

Muhtasari
  • Hii ni kashfa inayomzunguka rais Ramaphosa ya madai ya kuficha wizi wa sarafu za kigeni katika shamba lake la kibinafsi mnamo 2020
Rais Cyril Ramaphosa
Image: PSCU

Wabunge wa Afrika Kusini wamepiga kura kupinga ripoti ambayo inaweza kumuondoa madarakani rais Cyril Ramaphosa, karibu wanachama wote wa chama kinachotawala cha ANC wamemkingia kifua kiongozi wake.

Jumla ya kura zote ni:

Ndio- 148Hapana- 214Wasiokuepo - 2

Wabunge nchini Afrika Kusini walijadili ripoti inayoweza kumpelekea Rais Cyril Ramaphosa kuondolewa madarakani, kwa kuficha wizi wa kiasi kikubwa cha fedha za kigeni kwenye shamba lake.

Katika kile ambacho kilianza kama kikao chenye mvutano bungeni, spika wa bunge alikataa pendekezo la wabunge kupiga kura ya siri.

Hii ni kashfa inayomzunguka rais Ramaphosa ya madai ya kuficha wizi wa sarafu za kigeni katika shamba lake la kibinafsi mnamo 2020.

Hii ni kuhusiana na kashfa ya suala la shamba inayomzunguka rais, ambapo Bwana Ramaphosa ameshtakiwa kwa kuficha wizi wa sarafu za kigeni katika shamba lake la kibinafsi mnamo 2020.