June Chebet, bintiye Rais wa zamani Moi afariki

"Tuna huzuni kubwa kutangaza kifo cha mpendwa wetu, June Chebet Moi asubuhi ya leo," taarifa hiyo ilisema.

Muhtasari

• "Tuna huzuni kubwa kutangaza kifo cha mpendwa wetu, June Chebet Moi asubuhi ya leo," taarifa hiyo ilisema.

JUNE CHEBET
JUNE CHEBET
Image: HISANI

June Chebet, bintiye Rais wa zamani Daniel Arap Moi amefariki dunia.

Katika tangazo la Alhamisi, familia ilisema Chebet alifariki asubuhi.

Familia hata hivyo haijafichua maelezo zaidi kuhusu kifo chake, na kuomba faragha wakati wa maombolezo.

"Tuna huzuni kubwa kutangaza kifo cha mpendwa wetu, June Chebet Moi asubuhi ya leo," taarifa hiyo ilisema.

"Wakati huu wa majonzi, tunaomba dua na faragha yako wakati sisi familia tukipokea msiba wa dada yetu. Roho yake ipumzike kwa amani ya milele," iliongeza.

Taarifa zaidi zinafuata...