- Ufaransa yasajili idadi ya juu zaidi ya maambukizi tangu kuanza kwa janga
- Kuna hofu kwamba zuio la kuttoka nje litawekwa katika maeneo mengi
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza marufuku ya kutotoka nje katika mji wa Paris na miji mingine nane ili kuzuia usambaaji wa virusi vya corona
Kafyu hiyo ya kuanzia saa tatu usiku hadi saa kumi na mbili alfajiri itaanza kutekelezwa siku ya jumamosi na kudumu kwa takriban wiki nne Bwana Macronm ametangaza .
Hali ya dharura ya kiafya pia imetangazwa.
Kwingineko katika nchi ya Ujerumani serikali imetangaza kufungwa mapema kwa baa na mikahawa katika maeneo yenye hatari
Chansela Angela Merkel ametangaza vikwazo hivyo siku ya jumatano wakati taifa hilo liliripoti visa zaidi ya 5000 vya corona kwa mara ya kwanza tangu mwezi aprili .
Siku ya alhamsi idadi hiyo iliongzeka tena bvaada ya watu 6,638 kupatikana na virusi vya corona ambayo ndio idadi ya juu Zaidi tangu kuanza kwa janga la corona .
Chini ya sheria mpya , maeneo ambako maambukizi yatafika asilimia 50 kwa kila idadi ya watu laki moja yanafaa kufunga baa kufikia saa tano usiku .
Mikusanyiko ya watu binafsi inafaa kuwahusisha watu kumi pekee kutoka nyumba mbili .
Kote barani ulaya serikali za nchi hizo zimeanza kurejesha mikakati na vikwazo vya hapo awali huku pakizuka awamu ya pili ya maambukizi ya corona .
Kuna zuio la kutotoka nje katika baadhi ya sehemu za Uholanzi huku mikahawa na maeneo ya burudani ikifungwa .