Covid 19

Serikali huenda ikaweka vikwazo Zaidi baada ya ongezeko la maambukizi ya Corona

Ongezko la maambukizi lazua hofu

Muhtasari

 

  •  Tayarti shule kadhaa zimefungwa 
  • Kuna tatizo la watu kupuuza masharti 
  •  Sehemu nyingi za kazi zimerejelea hali ya kawaida 

 Hofu ya kuwepo  awamu ya pili ya maambukizi ya corona  huenda ikalazimisha serikali kuchukua hatua ya kuziisha vikwazo  ili kukabiliana na ugonjwa huo nchini .

 Hofu ni kwamba  maambukizi yamezidi katika kaunti nyingi zikiwemo Nairobi ,Mombasa  ,kiambu na Kajiado . idadi ya walioambukizwa ilipungua mwezi agosti na kuifanya serikali kulegeza masharti mengi lakini sasa takwimu zaonyesha kwamba idadi ya wanaoambukizwa inazidi kupanda kila uchao .

Shirika la afya duniani lilikuwa limeyaonya mataifa mengi duniani dhidi ya kulegeza masharti hayo lakini mengine yalikimbia kufungua chumi na shughuli za usafiri na sasa zipo katika njia panda  baada ya matokeo ya kuogofya kudhihirika kupitia ongezeko la maambukizi na maafa yanayotokea .

 Kenya ililegeza masharti yake septemba tarehe 28  wakati rais Uhuru Kenyatta alipotangaza kuanza kufunguliwa kwa awamu kwa sekta mbali mbali za uchumi na hata wanafunzi wa agredi ya 4,darasa la nane na kidato cha nne kuruhusiwa kurejea shuleni .

 Rais pia aliruhusu baa kurejelea oparesheni akitaraji kwamba  wahudumu wa maeneo hayo wangeweka mikakati ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo . Muda wa kafyu pia uliongezwa  ilia kuanza saa tano usiku hadi saa kumi alfajiri na hadi sasa bado kuna mjadala iwapo hatua hizo  zingechukuliwa kwa sababu miezi miwili baadaye hali imeanza kuwa tete .

 Serikali ilionekana kuwaachia wananchi jukumu la kujilinda wenyewe lakini  imedhihirika kwamba takriban nusu ya wananchi walirejelea shughuli za kawaida na kupuuza kabisa masharti yaliokuwa yamewekwa ili kukinga na kuwalinda wenzao .

 Huku taifa likipambana na janga la corona ,serikali pia ipo katika vita vya kukwamua uchumi  hatua ambayo ililazimisha  kufunguliwa kwa sekta mbali mbali za uchumi .

  Licha ya wizra ya elimu kusimama kidete na uamuzi wake wa kuzifungua shule kwa awamu ,tatizo limeibuka baada ya shule kadhaa kufungwa baada ya wanafunzi na walimu kupatikana na virusi vya corona . shule ya upili ya  Tononoka huko Mombasa ndio iliyoathiriwa Zaidi baada ya mwalimu wake mkuu Mohammed Khamis akuaga dunia siku ya jumatatu kwa ajili ya corona .