Nimekuwa nikifyatuliwa risasi kila ninapoenda kwenye kampeni-Bobi Wine

Muhtasari
  • Bobi Wine asema kuwa ameponea kifo mara mbili kwa muda wa wiki mbili
  • Pia alifichua kuwa amekuwa akivalia mavazi ya kuzuia risasi huku polisi wakimzuia kufanya kampeni kati miji mikubwa Uganda
aa02
aa02

Mgombea wa urais nchini Uganda Robert Kyagulanyi almaarufu Bobi Wine amefichua kwamba ameponea kifo kwa kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Akiwa kwenye mahojiano na runinga ya CNN alisema amekuwa akivalia vifaa vinavyozuia risasi kuingia mwilini mwake tangu alipoanza kampeni zake kwani maafisa wa jeshi wamekuwa wakifyatulia risasi gari lake kila anapokuwa kwenye kampeni.

" Nimeponea kifo mara mbili kwa muda wa wiki mbili iliyopita, nimekuwa nikifyatuliwa risasi kila ninapokwenda kwenye kampeni, inanilazimu nivalie bullet proof ili kuepuka majeruhi ya risasi, gari langu limefyatulia risasi kwenye gurudumu, vyioo zangu zimepasuliwa lakini najua hii ni siasa, tutashinda vita." Alisema Bobi Wine.

Kulingana na Bobi rais Museveni anajaribu kila awezalo ili kumzuia kuwania kiti cha urais.

Mwanamuziki huyo ambaye kwa sasa amegeuka kuwa mwanasisa amesema kwamba hatikisiki na hakuna uovu utakaomfanya akate tamaa.