Nyota wa YouTube wa Rwanda afungwa jela kwa kuwadhalilisha maafisa

Muhtasari
  • Nyota wa YouTube wa Rwanda amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela kwa kuikosoa serikali
Image: BBC

Nyota wa YouTube wa Rwanda amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela kwa kuikosoa serikali.

Dieudonné Niyonsenga, anayejulikana kama Cyuma au "Iron", alipatikana na hatia ya kughushi, uigaji na kuwadhalilisha maafisa wa serikali.

Anakanusha madai hayo na kusema atakata rufaa.

Video zake zimeshutumu askari kwa unyanyasaji mkubwa dhidi ya wakaazi wa makazi duni wakati wa marufuku ya kutoka nje katika kipindi cha janga la Corona

Mtu mwingine maarufu wa YouTube hivi majuzi alihukumiwa kifungo cha miaka 15 kwa kuchochea vurugu.

Mamlaka ya Rwanda mara kwa mara inashutumiwa kwa kukandamiza upinzani na kuwafunga jela wale wanaoikosoa serikali.

KWINGINEKO NI KUWA;

Waziri wa Mambo ya Ndani wa kwanza mwanamke wa Msumbiji ateuliwa

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi amemteua Arsenia Felicidade Felix Massinge kuwa waziri wa kwanza mwanamke wa Mambo ya Ndani nchini humo.

Pia amemteua waziri mpya wa ulinzi wa taifa, Cristóvão Artur Chume.

Mawaziri waliopita waliohusika na ulinzi na usalama wa ndani wote walifutwa kazi wiki hii.

Bw Chume ni Meja Jenerali anayejulikana kwa kuongoza vikosi vilivyokomboa miji mingi, ikiwa ni pamoja na Mocimboa da Praia katika jimbo la Cabo Delgado lililoathiriwa na wanajihadi.

Bi Massinge kabla ya kuteuliwa kwake alikuwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji.

Image: BBC

Pia amefanya kazi huko nyuma kama Kamanda wa Polisi wa mkoa katika mikoa ya Inhambane, Manica na Nampula.

Anatarajiwa kutumia uzoefu wake serikalini kukabiliana na changamoto nyingi zinazomkabili mtangulizi wake - ikiwa ni pamoja na ugaidi, ufisadi na utekaji nyara.