Jeshi la Uganda lakita kambi nje ya nyumba ya Bobi Wine kabla ya kampeni

Muhtasari
  • Jeshi la Uganda lakita kambi nje ya nyumba ya Bobi Wine kabla ya kampeni
Bobi Wine anasema kwamba anawakilisha vijana
Bobi Wine anasema kwamba anawakilisha vijana
Image: EPA

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi, al maarufu Bobi Wine, ametuma picha ya polisi na jeshi wakionekana nje ya nyumba yake kabla ya kampeni za uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika katika wilaya ya Kayunga.

Rais Yoweri Museveni anatarajiwa kutembelea katika wilaya ya Kayunga kumfanyia kampeni mgombea wa chama tawala anayewania nafasi ya uenyekiti.

Uchaguzi huo mdogo umepangwa kufanyika Alhamisi na chama tawala na upinzani kwa pamoja vinataka kuonyesha uwezo wao katika eneo hilo.

Bobi Wine ameshutumu jeshi na polisi kwa kujaribu kumzuwia kuondoka nyumbani kwake :

Vyombo vya habari nchini Uganda vimeripoti kuwa polisi na jeshi pia wamepelekwaKayunga kabla ya kampeni za Jumanne.

Awali Kayunga ilikuwa ni ngome ya chama tawala hadi mwenyekiti wa zamani aliyefarikiakiwa madarakani alipochaguliwa kutoka upinzani.

Chama tawala kinataka kurejesha tena kiti hicho na kimeahidi kuufanya mji huo kuwa manispaa, imeripoti gazeti la Daily Monitor.