Ukraine yawapa silaha wananchi 18,000 mjini Kyiv kupambana na Urusi

Muhtasari

•Mshauri wa wizara ya mambo ya ndani Vadym Denysenko anasema bunduki 18,000 "zimetolewa Kyiv kwa watu wote wa kujitolea, wale wote wanaotaka kulinda mji mkuu wetu kwa silaha mikononi mwao".

Image: AFP Via Getty Images

Wakati vikosi vya Urusi vikisonga mbele katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv mamlaka zinatoa wito kwa watu kufanya kila wawezalo kupinga uvamizi wa Urusi.

Wizara ya Ulinzi na Wizara ya Mambo ya Ndani inawaomba wakazi wa Kyiv "kutufahamisha kuhusu harakati za askari (adui)". Kipeperushi kilicho na maelekezo ya hatua kwa hatua ya jinsi ya kutengeneza mabomu ya petroli kimewekwa kwenye mitandao ya kijamii ya Wizara ya Mambo ya Ndani.

Mshauri wa wizara ya mambo ya ndani Vadym Denysenko anasema bunduki 18,000 "zimetolewa Kyiv kwa watu wote wa kujitolea, wale wote wanaotaka kulinda mji mkuu wetu kwa silaha mikononi mwao".

"Vifaa vya kijeshi vya Ukraine vikiwemo vifaru vinaingia Kyiv sasa ili kuilinda. Ninawataka wakazi wote wa Kyiv - tafadhali usiipige picha, usiipige picha harakati zoozote. Hii ni muhimu ili kulinda mji wetu."