Singapore yamnyonga mwanamume wa Malaysia mwenye akili punguani

Muhtasari
  • Kesi yake ilikuwa na utata mkubwa kwasababu alipimwa na mtaalam wa matibabu na kupatikana na IQ ya alama 69 - kiwango ambacho kinaonyesha ulemavu wa akili
Nagaenthran Dharmalingam alikuwa akisubiri kunyongwa kwa zaidi ya muongo mmoja

Mahakama nchini Singapore imemnyonga mlanguzi wa dawa za kulevya kutoka Malaysia, dada yake ameithibitishia BBC.

Nagaenthran Dharmalingam alikuwa akisubiri kunyongwa kwa zaidi ya muongo mmoja kufuatia hukumu aliyopewa kwa kujaribu kuingiza vijiko vitatu vikubwa vya dawa ya kulevya aina ya heroine nchini Singapore.

Kesi yake ilikuwa na utata mkubwa kwasababu alipimwa na mtaalam wa matibabu na kupatikana na IQ ya alama 69 - kiwango ambacho kinaonyesha ulemavu wa akili.

Lakini serikali ilisema "alielewa wazi asili ya kitendo chake".

Katika taarifa ya awali, serikali ilisema iligundua kuwa "hakupoteza hisia zake za uamuzi wa uzuri au ubaya wa kile alichokuwa akifanya".

Mahakama siku ya Jumanne ilitupilia mbali rufaa ya mwisho iliyowasilishwa na mama yake, akiongeza kuwa Nagaenthran alikuwa amepewa "utaratibu unaostahili kwa mujibu wa sheria", akiongeza kwamba "amemaliza haki zake za kukata rufaa na karibu kila njia chini ya sheria kwa muda wa miaka 11".

Katika kikao cha kusikilizwa kwa kesi yake siku ya Jumanne , Nagaenthran na familia yake walishakana mikono kupitia mwanya uliokuwepo katika ukuta mmoja wa glasi huku wakilia kulingana na ripoti ya Reuters. kilio cha 'Ma' kilisikika ndani ya mahakama.

Mwaka 2009, Nagaenthran alipatikana akivuka mpaka kuingia Singapore kutoka Malaysia akiwa na gramu 43 (1.5oz) za heroin iliyofungwa katika paja lake la kushoto.

Kwa mujibu wa sheria za Singapore, wale watakaopatikana na zaidi ya ghamu 15 za heroin watakabiliwa na adhabu ya kifo.

Wakati wa kesi yake, mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 34 alisema alishurutishwa kubeba dawa za kulevya, lakini baadaye akasema alifanya kosa hilo kwa sababu alikuwa anahitaji pesa.

Mahakama ilisema utetezi wake wa awali ulikuwa "wa kubuni". Hatimaye akahukumiwa kifo kwa kunyongwa.

Mwishowe, mahakama iligundua kuwa hakuwa na ulemavu wa akili. Shinikizo la mwisho la kuachiliwa kwa rais pia lilikataliwa mwaka 2020.

Mnamo mwaka wa 2015, aliomba hukumu yake ibadilishwe na kuwa kifungo cha maisha jela kwa msingi kwamba alikuwa na ulemavu wa akili.

Mawakili wake walikuwa wamedai kuwa kunyongwa kwa mtu mwenye akili punguani haifai chini ya sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Lakini mahakama iligundua kuwa hakuwa mlemavu wa akili. Msukumo wa kuhurumiwa kwa rais pia ulikataliwa mwaka jana.

"Mahakama ya Rufaa iligundua kuwa hii ilikuwa kazi ya akili ya uhalifu, ikitathmini hatari na faida zinazopingana zinazohusiana na tabia ya uhalifu inayohusika," ilisema Wizara ya Mambo ya Ndani ya Singapore katika taarifa ya awali.

Vuguvugu hilo limepata mvuto kwenye mitandao ya kijamii, ambapo kumekuwa na mirindimo isiyo ya kawaida ya hasira na huruma, ikiwa ni pamoja na bilionea wa Uingereza Richard Branson na mwigizaji Stephen Fry, wanaopinga adhabu ya kifo na wameitaka Singapore kuiokoa Nagaenthran.

Maelfu ya watu pia walikuwa wametia saini ombi, wakisema kwamba kunyongwa kwa mtu mwenye akilipunguani ni marufuku chini ya sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Hatua ya kunyongwa kwake siku yaJumanne ililaaniwa na shirika la kutetea haki za binadamu la Reprieve, ambalo lilimwita "mwathirika wa upotovu mbaya wa haki".

"Siku za mwisho za Nagen zilitumika, kama sehemu kubwa ya muongo uliopita, katika kutengwa kwa mateso kwa kifungo cha upweke," Mkurugenzi wa Reprieve Maya Foa alisema.

"Mawazo yetu yako kwa familia ya Nagen, ambayo haikuacha kumpigania; maumivu yao hayawezi kufikiria."

Mwanaharakati wa kupinga hukumu ya kifo wa Singapore Kirsten Han pia alitoa picha ya Nagaenthran siku ya Jumatano, ambayo iliripotiwa kuwa amevaa vazi lake alilopenda zaidi.

Serikali ya Singapore imesema kuwa sheria ya kimataifa haikatazi adhabu ya kifo na kwamba hakuna makubaliano ya kimataifa kuhusu matumizi yake.

Pia wamesema kuwa chini ya sheria za Singapore, hangepewa hukumu ya kifo iwapo mahakama ingempata "anasumbuliwa na tatizo la akili ambalo limeathiri kwa kiasi kikubwa wajibu wake kifikra".