Nina huzuni kuacha kazi bora zaidi duniani-Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson baada ya kujiuzulu

Anasema umma utahudumiwa kuanzia sasa hadi waziri mkuu mpya atakapochukua wadhifa huo.

Muhtasari
  • Johnson anasema ni upuuzi kubadilisha serikali – na kukataa wazo la uchaguzi mkuu - wakati ‘’tunatimiza majukumu mengi na makubwa hali ya kiuchumi ikiwa ngumu sana ndani na kimataifa’’.
Image: BBC

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amejiuzulu wadhifa wake. Akitoa hotuba yake alisema:

''Ninasikitika kuacha kazi nzuri zaidi duniani lakini ndiyo hali halisi''

‘’Ninataka ujue jinsi ninavyohuzunishwa na kuacha kazi bora zaidi duniani,’’ waziri mkuu anasema.

"Nimekubaliana na Sir Graham Brady, mwenyekiti wa wabunge wetu wa viti maalum, kwamba mchakato wa kumchagua kiongozi mpya uanze sasa na ratiba itatangazwa wiki ijayo. Na leo nimeteua Baraza la Mawaziri kuhudumu, pia nitaendelea kuongoza hadi kiongozi mpya atakapochaguliwa.’’

''Inatia uchungu kutoona miradi yangu ikikamilika''

Johnson anasema ni upuuzi kubadilisha serikali – na kukataa wazo la uchaguzi mkuu - wakati ‘’tunatimiza majukumu mengi na makubwa hali ya kiuchumi ikiwa ngumu sana ndani na kimataifa’’.

‘’Najuta kutofanikiwa katika majadiliano na inatia uchungu kutoona mawazo na miradi mingi ikitimia.’’

Bwana Johnson ameshukuru umma kwa ‘’mapendeleo makubwa’’

‘’Zaidi ya yote, ninataka kuwashukuru nyinyi, umma wa Uingereza, kwa mapendeleo makubwa mliyonipa,’’ amesema.

Anasema umma utahudumiwa kuanzia sasa hadi waziri mkuu mpya atakapochukua wadhifa huo.

Mustakabali wetu pamoja ni uliong’aa - Johnson

Waziri mkuu amemaliza kauli yake kwa kusema kwamba hadi pale atakapopatikana mbadala wake, maslahi ya umma yatatekelezwa.

‘’Kuwa waziri mkuu ni elimu ya kivyake - nimesafiri kila sehemu ya Uingereza na nimekutana na watu wengi wenye asili ya Uingereza isiyo na kikomo na wako tayari kushughulikia matatizo ya zamani kwa njia mpya.

‘’Hata kama mambo yanaweza wakati mwinginekuonekana kuwa giza nene, mustakabali wetu pamoja ni mzuri, uliong’aa,’’ Johnson anasema huku akipigiwa makofi anapoondoka.