Mzozo wa Sudan: Pande zinazopigana zakubaliana kusitisha mapigano kwa siku 7

Kama sehemu ya hatua hiyo, maafisa wa Sudan wamekubaliana kurejesha huduma muhimu

Muhtasari

•Makubaliano ya awali ya jeshi na kikundi cha wanajeshi wa dharura -Rapid Support Forces (RSF) yamekuwa yakikiukwa katika kipindi cha dakika chache kabla ya utekelezaji wake kuanza.

Zaidi ya watu milioni wanakadiriwa kuzikimbia nyumba zao tangu vita vianze
Image: BBC

Pande mbili zinazopigana nchini Sudanzimeafikiana kusitisha mapigano kwa muda baada ya mapigano hayo kuendela kwa wiki ya sita.

Makubaliano ya awali ya jeshi na kikundi cha wanajeshi wa dharura -Rapid Support Forces (RSF) yamekuwa yakikiukwa katika kipindi cha dakika chache kabla ya utekelezaji wake kuanza.

Lakini mkataba mpya utaimarishwa na "mpango wa ufuatiliaji wa usitishaji wa mapigano," kulingana na taarifa ya Marekani na Saudi Arabia.

Kama sehemu ya siku saba za usitishaji huo wa mapigano wa kibinadamu , maafisa wa Sudan wamekubaliana kurejesha huduma muhimu.

Mapigano baina ya pande mbuili yameliingiza taifa katika limbi la ghasia tanfu yalipoanza mwezi uliopita, huku zaidi ya watu milioni wakidhaniwa kuyakimbia makazi yao.

Akiba za chakula, pesa na huduma muhimu vimepungua kwa haraka na makundi ya misaada yamekuwa yakilalamika mara kwa mara kuwa yameshindwa kutoa usaidizi wa kutosha katika mji mkuu wa SudanKhartoum, ambako kuna ghasia zaidi