Mkuu wa jeshi la Israel aapa kulipiza kisasi shambulizi la Iran

Nevatim, aliwaambia wanajeshi wa angani kwamba hatua ya Iran kurusha makombora haiwezi kuachwa kupita bila kujibiwa.

Muhtasari

• Changamoto kwa baraza la mawaziri la vita ni kutafuta njia ya kutoa ujumbe mkali bila kuchochea mgogoro wa kikanda.

Image: BBC

Viongozi wa Israel wanaonekana kuhitimisha kuwa ili kuidhibiti Iran ipasavyo, ni lazima walipize kisasi shambulio lake kubwa la makombora.

Akitembelea kambi ya anga ya Nevatim, ambayo iliharibiwa kidogo na shambulio la Iran, mkuu wa jeshi la Israel, Herzi Halevi, aliwaambia wanajeshi wa jeshi la anga kwamba hatua ya Iran kurusha msururu wa makombora haiwezi kuachwa kupita bila kujibiwa.

Changamoto kwa baraza la mawaziri la vita ni kutafuta njia ya kutoa ujumbe mkali bila kuchochea mgogoro wa kikanda.

Iran ilifanya shambulizi lake ambalo halijawahi kushuhudiwa kulipiza kisasi kwa shambulio baya la anga jumba ladhidi ya ubalozi wake mjini Damascus, ambalo linadaiwa kufanywa na Israel, na imeashiria kwamba haina nia ya kuendelea na mashambulizi zaidi.

Viongozi wa dunia wameelezea hofu kwamba sasa kuna uwezekano wa vita vya wazi zaidi kati ya mahasimu hao wa muda mrefu na ghasia zinazotokana na vita vya Gaza kuenea zaidi.