Mwanamke auawa kwa kudungwa kisu na 'landlord' South C, familia yalilia haki

Mwanamke huyo alikuwa mfanyikazi wa kusafisha ambapo mwanamke mwenye nyumba aliyempa kazi anadaiwa kumdunga kisu kabla ya kumtupa nje ya boma.

Muhtasari

• Marehemu alikuwa mama wa watoto watatu na mjane kufuatia kifo cha mumewe miaka mitatu iliyopita.

Crime scene
Crime scene
Image: MAKTABA

Familia moja inayoishi katika mtaa wa mabanda wa Kibera inalilia haki baada ya mpendwa wao kudaiwa kuuawa kwa kudungwa kisu na mwenye nyumba alikokuwa amekodisha kuishi.

Mwanamke huyo ambaye sasa ni marehemu kwa jina Anastacia Katumbi, 37, alidungwa kisu na mwenye nyumba mnamo Novemba 22 katika eneo la South C. Mwanamke ambaye ni mwenye nyumba katika eneo hilo alikuwa amempa kazi ya kusafisha na baada ya mzozano kiasi alimdunga kisu na kumuua.

Kulingana na Nation, Bi Katumbi alisaidiwa na mwanamke ambaye familia ilimtaja tu kama Mama Weru, ambaye alimkimbiza katika zahanati ya eneo hilo kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya Mbagathi katika Kaunti Ndogo ya Lang’ata.

Mama Weru alisema kuwa alimuona mwanamke huyo akihangaika kwa maumivu, ndipo akaamua kumkimbiza hospitalini baada ya kutupwa nje ya boma hilo.

“Niliigiza tu nafasi ya msamaria mwema ambaye alikuwa amejitolea kuokoa maisha. Nimeambiwa kutoka huko alipelekwa katika Hospitali ya Mbagathi na baadaye akapewa rufaa ya Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta,” Nation ilimnukuu/.

Sasa imeibuka kuwa marehemu alikuwa mama wa watoto watatu na mjane kufuatia kifo cha mumewe miaka mitatu iliyopita.

Ana mtoto wa kwanza wa kiume, mwenye umri wa miaka 26, binti wa pili, mwenye umri wa miaka 22, na mzaliwa wake wa mwisho ana umri wa miaka 15.