'Anayeeneza uvumi huo sio mtu mzuri,'Baba yake DJ EVolve akana madai kuwa mwanawe ameaga dunia

Muhtasari
  • Baba yake DJ EVolve akana madai kuwa ameaga dunia
  • Aliongeza na kusema kwamba anaye eneza uvumi huo au habari hizo sio mtu mzuri

Baba yake mcheza santuri DJ Evolve, Felix Orinda amekana madai kwamba mwanawe ameaga dunia.

Orinda akiwa kwenye mahojiano na mpasho, alitupilia mbali madai hayo na kusema kwamba mwanwe yuko hai.

Aliongeza na kusema kwamba anaye eneza uvumi huo au habari hizo sio mtu mzuri.

"Yuko sawa, kifaa kilichowekwa katika koo yake kiko bado, lakini hajaanza kuongea vyema nimepigiwa simu na mwanahabari mwingine kuhusu uvumi huo

Anyeeneza habari hizo sio mtu mzuri, mtu anaye tangaza kifo cha mtu akiwa hai, huyo ni mtu wa aina gani? huyo sio mtu mzuri nimempigia mwanangu amabaye anaishi na yeye ameniambia yuko sawa," Aliongea.

Mapema mwaka huu akiwa kwenye mahojiano na radiojambo baba huyo alisema kwamba Babu Owino amekuwa akigharamikia matibabu ya mcheza santuri huyo.

"Siku moja kabla ya ajali yake nilimpigia felix simu ni kamwambia aje kuniona,alipokosa kuja kuniona nilijua kwamba amezidiwa na usingizi

Asubuhi nilipokea simu na nikaambiwa niende katika hospitali kuwa mtoto wangu yuko hosptali, nilipofika Felix alikuwa anaongea na hata kucheka alikuwa anacheka

Baada ya hapo siku iliyofuatia Felix alinyamaza hadi miezi mitano, Babu Owino ndio anasimamia Gharama za DJ Evolve hadi leo,alikuwa anaendelea vyema lakini hivi majuzi amepatwa na shida lakini ,madaktari wanashughulika," Alieleza Baba Evolve.

DJ Evolve alivuma kwa muda kwenye mitandao ya kijamii baada ya kupigwa risasi na mbunge wa Embakasi mashariki.