Mama mkwe Dikteta

Nimefika mwisho! Mume wangu hufuata kila anachoambiwa na mamake

Imekuwa vigumu uamuzi wa ndoa kufanywa bila mchango wake

Muhtasari

 

  •  Kuna  mama wakwe wasiojua mipaka yao katika maisha ya watoto wao
  •  Kama mwanamke dumisha heshima lakini pia simama kidete kuhusu yafaayo na yasiokufaa
  •  Elizabeth anasema huenda akamuacha mumewe sio kwa kutompenda bali kwa ajili ya muingilio wa mama mkwe 

 

Ndoa  ukiwa nje huonekana kuwa kitu kizuri sana na  hakuna mabaye huweza kutabiri au kujua baadhi ya changamoto ambazo zinaweza kuleta msukosuko katika uhusiano kati ya  mume na mke .

 Wakati watu wanapofanya mipango ya kufunga pingu za maisha ,wengi hujua kwamba basi wamefika mwisho kuhusu  kuwahi kumtafuta mtu mwingine wa kuwahi kuishi naye maisha yao yote .wengia wakati huo wa mwanzo mwanzo huwa hawafikirii kwamba  wakati mwingine kuna sababu au watu wengine ambao huweza kuwa na  ushawishi mkubwa wa kutengeza ama kuvunja ndoa yao .

  Kwa Elizabeth   Kawira* amejifunza hilo akiwa ndani ya ndoa baada ya  kubainika wazi kwamba  uhusiao wake na mama mkwe wake hautawahi kuboreka kwa sababu  mama mkwe ndiye amekuwa akiendesha kila hatua katika maisha yao .

 Elizabeth anasema walipoona na  Francis, hapakuwa na ishara kwamba mamake atakuwa na usemi kupindukia katika maisha yao na kila jambo lilionekana  kuwa la kawaida ila muda ulipozidi wakiwa katika ndoa ,amegundua kwamba  maamuzi yote kuhusu maisha yao lazima yaidhinishwe na mama mkwe kwani  Francis hawezi katu kufanya lolote kabla ya kushauriana na mamake kwanza .

   Elizabeth anasema mtindo huo wa ndoa yao umekuwa ukivuruga uhusiao  kati yake na  mume wake kwa sababu  wakati mwingine yaonekana ni kana kwamba ndoa yao ni mume moja na wake wawili . Mama mkwe ndiye aliyeamua shule ambako mtoo wao wa kwanza alipelekwa na hata gharama ya shule . Anapokuja kuwatembelea ,mama mkwe huamua kila chakula wanachoandaa  na Elziabeth anahisi sasa kwamba mama ya mume wake anamsakama na kuivuruga ndoa yake .

  Anaogopa kumzungumza na mume wake kuhusu tabia za  mamake kwani anasema juhudi zake za kumuelea kuhusu baadhi ya vitendo vyake vya kumhusisha mamake katika masuala yao  havipendezi zimefeli na alichukulia kwa ubaya kwani aliona ni kana kwamba mke wake alikuwa analenga kumtenganisha na  mamake .

  Mama mke amekuwa akitoa matamshi ya kushangaza wakati mwingine na  msimamo wake kuhusu mambo hayo haujakuwa ukimpeneza Elizabeth . kwa mfano ,mpango wa Elizabeth na mume wake kufungua akaunti ya pamoja ya benki ili kuaza kuweka akiba ya waoa siku za baadaye ulitibuka wakati Francis alipomueleza mamake kuhusu  hilo . Mamama mke  alifoka sana akidai Elizabeth alikuwa na njama  za kuiba pesa za mwanawe na hivyo ndivyo mipango yao mingi ilivyofeli .

  Anasema anampenda mume wake na hana nia ya kuondoka lakini kutokana na jinsi mama mkwe alivyowasakama kwa kuingilia kila uamuzi na hatua wanazofanya ,huenda akalazimika kuchukua hatua  kal na hivi karibuni atalazimika kumtaka mumewe achague kati yake na mamake .