Kula 'fare'

Masaibu: 'Nilikula fare ya mwanamume, sikujua ilikuwa ya pastor wangu’

Usijarimu kumlaghai mtu usiyemjua

Muhtasari
  •  Imekuwa mtido kwa wanawake 'kula fare' lakini Cathy hakujua yaliomngoaj 
  •  Anasema kisa hicho kimemshtua na hawezi sasa kumlaghai mwanamme yeyote 
  •  Cathy alishangaa kwamba mhubiri wake ambaye ana mke ,aliweza kumtumia shilingi 5000 

 

Cathy  Warigo* amejipata katika hali ambayo  wengi wanamcheka sana kwa sababu katika mzaha wote unaotawala mitandao ya kijamii na lalama za wanaume kuhusu  wasichana kuwalaghai pesa wanaume kwa kutumiwa nauli na kukosa kuja kama wanavyoahidi ,yeye alichukua persa za mtu ambaye hakumdhania anaweza kuwa pia mwathiriwa katika  ‘lalama’ hizo .

 Kote pamekuwa na visa vingi vya wanaume kulalamika kwamba baada ya kutongozana na msichana katika kumbi hizo za mitandao ,wengi huitisha pesa wakisema ndio ‘nauli’ ya kufanikisha  safari yao ili kwenda ‘date’ au hata kuja majumbani kwa wanaume kuwatembelea-unajua hilo linamaaniha nini.

  Masaibu ya Cathy yalianza wakati mtu mbaye hakumjua alipoanza kumtumia ujumbe wa mapenzi kupitia facebook . Yamkini alivyozungumza yule mtu  katika jumbe zile alionekana kumjua vizuri sana Cathy . Juhudi za Cathy kumataka ajitambulishe ziliamulia patupu kwa sababu hata jina lake katika facebook halikuwa halisi na pia alikuwa tu ameweka picha ya gari na hivyo basi ilikuwa vigumu kujua ni nani .

 Kama wanavyofanya wanawake wengi Cathy aliamua kujiambia kwamba basin aye pia atajiunga na mamia ya wanawake ambao wanafanya mazungumzo ya muda mrefu na wanaume katika mitandao kisha baadaye wanakula pesa zao na kuingia mitini kwa sababu asiyekuajua uko wapi atakupataje?  Muda uliendelea  na Cathy akizungumza na jamaa huyu ambaye wakati wote asubhi anaamkia kwa kumtumia jumbe za  kumjulia hali ,akimuuliza usiku wake umekuwa vipi au siku yake imekuwa vipi na baadaye wakaunda mazoea kana kwamba ni watu wanaoajuana . Ilifika wakati wakaanza hata kuitana majina matamu tamu ya mapenzi kama  ‘Dear,Babe,Honey’ na kadhalika .

 Siku ya siku ilipofika basi ikawa inachofuatia ni wao kukutana ana kwa ana kwa sababu katika fikra za yule mwanamme  ,tayari yeye na Cathy walikuwa katika uhusiano .

 Wakakubaliana kuhusu Cathy kwenda kwake na  hata matayarisho yakafanywa kuhusu watakavyokutana . Ikawa sasa jamaa amesema Cathy asiwe na wasi wasi kuhusu kugharamika kwa safari hiyo kwani yeye atalipia kila gharamana angemtumia pesa kupitia nambari yake ya simu . Yakapigw amahesabu kwamba zilihitajika shilingi 5000 kama ‘nauli’ pamoja na  gharama za chakula akiwa safarini .

 Jambo ambalo  Jamaa yule hakujua ni kwamba Cathy hakuwa na mpango hata kidogo wa kwenda kukutana naye . Alipotumiwa zile pesa alizitoa kwenye simu yake na kisha kuiblock nambari ya jamaa yule ili asiweze kuwasiliana naye . kwa ufupi Cathy alikuwa kashakula fare  kama wanavyosema wakenya kuhusu ulaghai wa wanawake kuchukua pesa za wanaume na kisha kudinda kutekeleza ahadi wanazotoa .

 Cathy hakujua kwamba mshangao ulikuwa unamngoja  na baada ya ushindi wake wa kukatalia pesa za mwanamme  siku ya ijumaa  kisha akazima simu yake jumamosi nzima ,jumapili ilikuwa siku ya kwenda kanisani .

 Kama kawaida alijitayarisha na watu wengine wa familia na kwenda katika kanisa lao la kawaida na bila kujua ,mhubiri wao mkuu kwenye kanisa hilo alimuita kando baada ya sala na kumtaka arejeshe pesa zake ambazo alimtumia !

 Cathy alishangaa siweze kujua ni vipi mhubiri huyo alivyojua kwamba ametumiwa pesa lakini haikuchukua dakika moja kabla hajagundua kwamba mtu ambaye amekuwa akizungumza naye kwenye facebook kwa muda huo wote na aliyemtumia zile pesa alikuwa pastor wake pale kanisani!