Mambo ambayo wanaume wanaangalia kwa wanawake zaidi ya sura nzuri

Ndio lazima wanaume wengi waangalie sura ya mwanamke ambaye anataka awe mpenzi wake lakini kuna mambo zaidi ya sura nzuri na urembo ambao wanaangalia ili kuhakikisha kuwa maisha yao yatakuwa sawa licha ya changamoto za kawaida.

Kati ya mambo ambayo wanaume wengi uangalia ni kama vile yafuatayo;

1.Ujuzi wa kupika

 

Kuna wanawake ambao wana sura nzuri lakini hawana ujuzi wa kupika kama ni sukuma anakaanga tu kama kawaida hawezi ongeza viungo vingine.

Hii ni jambo muhimu sana katika uhusiano na ndoa lakini inawaendea 'slayqueens' ambao kazi yao ni kujirembesha na kujipodoa ili waonekane warembo na waume wao.

2.Tabasamu

Si kila mara unapotembea unaweka sura ya kazi wakati mwingine tabasamu kidogo, pia wajue kwamba unatabasamu nzuri.

3.Ucheshi

Kuna wakati mwanamume wako anataka ucheke ucheshi wake si kila mara tu ni kuzuungumzia mambo muhimu.

4.Utunzaji wao

 

Mtunze mume wako na umuonyeshe mapenzi tele, je usipomtunza atatunzwa na nani?

Pia wanaume nao wanahitaji kutunzwa.

5.Kuwa halisi na asili

Kama mwanamke kama mwanamume wako anakupenda au umetambua kuwa kuna mwanamume anakupena haya basi kuwa halisi usiishi maisha ya mtu mwingine bali kaa maisha yako.

6.Silika za kimama

Wanaume ambai wanatambua maisha yao pia nao wana maono ya kesho kuwa na familia na watoto kwanini usiwe na silika za kimama kwa maana siku moja nawe pia utakuja kuwa mama.

7.Kuweza kukubaliana

Si kila mara wewe mwanamke ndio wapaswa kusikizwa na kupewa muda wa kuzungumza haya basi mpe mwanamume wako wakati naye azungumze na mkubaliane kwa jambo fulani.

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo wanaume wengi uangalia katika maisha ya mwanamke zaidi ya sura nzuri.