Mambo ya simu ya mkononi

Kisimu cha mkono kilivunja ndoa yangu

Kunazo ndoa zimevunjika kwa sababu ya simu ya mkononi ambayo sasa ni sumu katika ndoa .

Muhtasari
  • Aliposoma na kuona wote waliokuwa  wakiwasiliana naye hakutaka kupata majibu alifungisha virago vyake na kuondoka .
  • Sasa kunao wanawake  ambao  wamejipa busara ya kusema ,ugonjwa  ambao haunipi uchungu basi sina haja ya kujua unaitwaje.

 

 

Ni kifaa kidogo cha mkononi ambacho kilifaa kurahisisha mawasiliano  miongoni mwa watu . Lakini sasa iwapo kuna njia rahisi ya kuvunjika kwa ndiooa ama sababu  kubwa ya kuvunja mahusiano basi simu ya mkonoi imetajwa kuwa nambari moja katika orodha hiyo

Wengi wanajutia au hata kufurahi kwa uamuzi wao wa kujipata wakchungulia jumbe na mawasiliano ya wenzao katika simu zao wa mkononi lakini jambo ambalo hawakulipangia ni matokeo yake .

Ndio hali ambayo  Bity  Wariama amejikuta kwani kila siku anaishoi akijiambia kwamba laity angelijua basi hangepambana kwa udi na uvumba kuichukua simu ya mume wake na kuangalia jumbe zake zote ! Aliposoma na kuona wote waliokuwa  wakiwasiliana naye hakutaka kupata majibu alifungisha virago vyake na kuondoka .

Tatzio ni kwamba , sasa miezi kadhaa badaye alipofahamu kwamba kuna wanawake wengi waliokuwa wakiwasiliana na mume wake naye hakuwa na haja bali alikuwa tu akiwajibu kwa minajili ya mazungumzo  Bity alianza kujuta na kufikia wakati huo ,mume wake alikuwa ashaamua kwamba Bity ana akili za  kitoto na basi akasonga mbele na maisha yake kwa kupata mke mwingine .

 Hadi leo kuna visa vingi ambavyo marafiki ,jamaa katika familia na hata viongozi wa kidini wanapatanisha wana ndoa kuhusu mambo ya kuichukua simu ya mwenzio ili kutaja kujua yaliyomo . Wengi wanashauri kwamba kila mtu azingatie mambo yake na simu yake . Simu ya mwenzio usiwe na uchu wa kutaka kujua yaliyomo kwa sababu kwa mfano kama mwanamke ,ukitaka kupata ushahidi kwamba kuna mwanamke mwingine anawasiliana na mume wako basi utapata .  Sasa kunao wanawake  ambao  wamejipa busara ya kusema ,ugonjwa  ambao haunipi uchungu basi sina haja ya kujua unaitwaje. Wao hawana haja ya kuziangalia simu za waume zao kwa sababu wanaogopa kupatwa na mshutuko wa moyo bure  .

Lakini pia kunao wenye dhana kwamba iwapo katika ndoa hamfichani lolote au hakuna anayefanya mabaya huko nje ,hamna haja ya kuificha simu yako ili mwenzako asione jumbe au simu unazopiga .Sasa kuna tofauti  hapo ya jinsi kila walio katika ndoa wanavyoendesha mambo yao hasa kuhusiana na masuala ya simu ya mkononi . Kunazo ndoa zimevunjika kwa sababu ya simu ya mkononi ambayo sasa ni sumu  katika ndoa .Je,inafaa kuwa vipi? Unafaa kumruhusu mwenzako kuishika simu yao na kuchakura kusoma jumbe zote? Kuna vituko vingi kuhusu hili na hata kunavyo visa vya wanaume kwenda bafuni na simu ya mkononi au hata kuizima kabla ya kwenda bafuni  na wengine wana  passwords ndefu na ngumu kama kutokea Timbuktu hadi Kabwodo .