Kiungu mkuti

Tuliachana na mume wangu alipokataa nisifanye kazi

Muhtasari
  • Angenichagulia nguo ambayo ningevaa nikienda  kazini ….wakati  mwingine nikijipodoa angesimama kando ya kioo akishangaa mbona najipodoa sana’ anasema Lisa
  • Kwa takriban mwezi mmoja alikuwa amenuna  na hakuna aliyekuwa akizungumz ana mwingine .

 

Wakati mwingi pana migogoro kati ya wanandoa kuhusu  mwanamke kufanya kazi .Ingawa kuna wanaume ambao hawana tatizo na wake zao kufanya kaiz ,kuna idadi kubwa ya wanaume ambao hupata tatizo sana na hata kupinga hatua ya wake zao kutaka kuwa na kaz

Lisa Njeru  anasema  ndoa yake ilivunjika na hana majuto baada ya mume wake  Richard kukataa kabisa kwamba asifanye kazi .  Pingamizi yake kubwa ilitokana na hali yake ya kuwa na wivu na kuhofia kwamba  Lisa angekutana na mwanamme mwingine aliye ora huko kazini . Kila alipokuwa akitoka kazini ,Lisa anasema angempata mume wake amemngoja huku akiwa na maswali chungu nzima kuhusu watu aliokuwa amezungumza nao akiwa kazini

‘Angenichagulia nguo ambayo ningevaa nikienda  kazini ….wakati  mwingine nikijipodoa angesimama kando ya kioo akishangaa mbona najipodoa sana’ anasema Lisa

Anasema   mwanzoni alifikiri labda hali ingeboreka na mume wake atulie kwa sababu hakuwa amewahi kufanya lolote la kumpa shauku au hofu kuhusu mapenzi yao . Lakini ilipofika  wakati Lisa alipopandishwa cheo ili kuwa mkuu wa idara yake ,mume wake alimpa makataa ya kuacha kazi .

 ‘Aliniambia bila kusita kwamba amefika mwisho na nifanye uamuzi kati ya hiyo kazi na ndoa yangu’ Lisa anasema

 Baada ya kujaribu kuzungumza na kakake za mume wake wajaribu kuongea na  ndugu yao kuhusu mzozo huo  Richard hakubadilisha msimamo na kwanza alikerwa Zaidi na hatua ya Lisa kuwahusisha jamaa zake katika suala hilo . Kwa takriban mwezi mmoja alikuwa amenuna  na hakuna aliyekuwa akizungumz ana mwingine .

Baada ya kufirikia hatua atakayochukua ,Lisa alifanya uamuzi ,alifungisha virago vyake na kuondoka .Kilichomfanya kukwera Zaidi ni matamshi ya mume wake kwamba  Lisa alikuwa na   kiburi kwa sababu ya kazi na cheo chake . Alifahamu kwamba iwapo angeiacha kazi na tabia zile za Mume wake ,bado ndoa yao ingekuwa tu katika mizani na siku moja lingelipuka bomu ambalo lingemuacha bila ndoa au njia ya kujipa kipato . Je,Mbona kuna wanaume wasiotaka wake zao wafanye kazi?