Mambo ambayo yanaweza fanya uhusiano wako wa kimapenzi kudumu

Muhtasari
  • Mambo  madogo ambayo yanaweza fanya uhusiano wako wa kimapenzi kudumu
  • Katika kila uhusiano lazima kuwe na panda shuka za kila aina

Ukweli ni kuwa kabla ya wanandoa kufika kiwango cha ndoa lazima wapitie kiwango cha uhusiani wa kimapenzi ili wajuane na kufahamiana vyema.

Katika uhusiano huo utajua mpenzi wako anapenda lipi na hapendi lipi.

Kuna mambo kadha wa kadha ambayo watu upuuzilia mbali ambayo yanaweza uhusiano wao kudumu milele.

Lakini mambo hayo ni kama gani?

1.Wacha yaliyopita yakuwe yaliyopita

Kama waaka uhusiano wako hudumu kama mmeanza kukeleleshana na mpenzi wako husijaribu kuleta maneno ya kale ambayo yalifanya mkosane hayo yapuuzilie na kisha uendelee na kuyasahau.

2.Panga siku ya kufanya mapenzi

Kama mwanamume si kila siku unakuja na hamu ya kufanya mapenzi ilhali mke wako yuko katika suiku zake za hedhi, mkiwa wawili pangeni ni siku na wakati upi mnapaswa kufanya hayo.

3.Tazama sinema pamoja

Usijipende sana kana kwamba utatazama sinema ambayo pia mpeni wako anaipenda pekeyako, ilhali yeye yuko jikoni anakutayarishia chakula.

 

Ngoja amalize ili muweze kutazama pamoja.

4.Usipange lolote bila mwenzako

Ndio lazima kila mtu awe na mipangilio maishani mwake, lakini endapo waenda kupanga lolote au chochote na una mpenzi haya basi mfahamishe ili naye ajue jinsi atajipanga, si kuja leo na kumwambia kuwa wataka jambo fulani.