Mambo ambayo kamwe hupaswi kumwambia rafiki yako ambaye amepewa talaka

Muhtasari
  • Kila wanandoa wanapofunga pingu za maisha huwa na matumaini kwamba watatenganishwa na kifo
  • Mambo ambayo kamwe hupaswi kumwambia rafiki yako ambaye amepewa talaka

Kila wanandoa wanapofunga pingu za maisha huwa na matumaini kwamba watatenganishwa na kifo.

Lakini mambo hutendeka huku wengi wakipeana talaka, na hata kujuta kwanini walifunga pingu za maisha.

Endapo mtu anapitia mchakato wa talaka huwa hasemi wala kuungumzia swala hilo kwani kuna wale huwa wameumia moyo.

Lakini zaidi ya yote, kuna mambo ambayo hupaswi kumwambia rafiki yako kama anapitia au ametalikiana na mumewe au mkewe.

Mambo hayo ni kama;

1,Unapaswa kumrudia

Ukiona wametalikiana inaonyesha kwamba walijaribu kila kitu wawezalo ili uhusino na ndoa yao iweze kudumu lakini likashindikana.

Kwa kauli au jambo kama hilo haupaswi kumwambia mtu mabaye ametalikiwa.

2.Nilimuona mume au mke wako na mpenzi mwingine

Labda hajasahau yale alipitia katika uhusiano na mpenzi wake au bado ana hisia zake kwa maana hajasahau mapenzi yake, ni jambo ambalo ata ukimuona mpenzi wake na mpenzi mwingine unapaswa kunyamaza ili ajionee mwenyewe.

3.Ni jambo la kuhuzunisha hamkuweza kudumisha uhusiano wenu

Ndio walijaribu, na kama huo sio ubavu wako hauwezi lazimisha, na mapenzi hayalazimishwi.

4.Ndoa yangu pia sio nzuri vile

Wakati huo jiekee shida zako kwa maana mwenako anapitia hali ngumu na anahitaji kusikia mambo ya kumtia moyo wala sio kumvunja moyo.

Tumewaona na kuwasikia marafiki zetu kuwa wameapana talaka na mumewe au mkewe, na hata watu mashuhuri tumewaona wakiachana, lakini kama rafiki unapaswa kujua na kufahamu cha kusema wakati wa hali hiyo ngumu.