Fahamu jinsi ya kuimarisha uhusiano wa kimapenzi uzeeni

Muhtasari

•Kujamiiana ni sehemu muhimu sana kwa ustawi wa wazee (93%), na ingawa hali ya kuingiliana kimwili hupungua, asilimia 71 ya wazee hufurahia mapenzi na asilimia 69 kati yao hupata hisia kali.

Image: GETTY IMAGES
Image: GETTY IMAGES
Image: GETTY IMAGES

Raha haipungui kutokana na umri

Baadhi ya wazee huendelea kufanya ngono, kwani hamu ya kujamiana na raha haipungui kutokana na umri.

Ingawa umri, peke yake, sio sababu ya kumfanya mtu kubadili mwenendo wake wa maisha ambayo yamekuwa yakifurahia, kuna haja ya kubadili mtindo wa maisha wakati hali inapomlazimu mtu kufanya hivyo, kwa mapungufu fulani ya kimwili na madhara ya magonjwa au dawa.

Katika tamaduni nyingi, ngono inahusishwa na vijana hali ambayo inaweza kuwafanya wazee kuhisi kutengwa. Dhana hiyo pia inaweza kuwaathiri kisaikolojia wakashindwa kushiriki tendo la ndoa.

Lakini wataalamu wanasema: "Ngono katika miaka ya uzeeni inasisimua mwili na kuusaidia. Tuna wakati wa kutosha kujiburudisha na ni vyema kuwa na mbinu tofauti za kufanya hivyo,"

Kulingana na matokeo ya utafiti iliyofanywa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Wazee (UCLM, Albacete 2020), kujamiiana ni sehemu muhimu sana kwa ustawi wao (93%), na ingawa hali ya kuingiliana kimwili hupungua, asilimia 71 ya wazee hufurahia mapenzi na asilimia 69 kati yao hupata hisia kali.

Image: GETTY IMAGES

Claudia na Luis walikutana wakiwa vijana. Walipendana sana na kila mmoja alikuwa akimuwaza mwenzake walipokuwa mbali mbali na walipokutana miili yao ikasisimka kwa kusuguana tu. Walifurahia kufanya mapenzi mara kwa mara.

Wamekuwa pamoja kwa muda mrefu. Ingawa wanakabiliwa na chnagamoto za kifya, kimsingi wamefanikiwa kujitunza vyema na kujudhibiti.

Wanatumia muda, kwenda kwa matembezi na kushiriki kazi za nyumbani. Mara kwa mara, pia wanawatunza wajukuu wao. Licha ya umri wao mkubwa bado wanapendana! Ila sasa wanapendana kwa namna tofauti kwa namna tofauti, wakifurahia kuwa pamoja na kuliwazana.

Kila binadamu ambaye ameshazoea kuwa karibu na mwenza wake siku zote angependa iwe hivyo. Hii ni pamoja na kuendelea kuwa na hamu ya tendo la ndoa, uwezo wa kufanya tendo la ndoa na kuridhishwa na tendo la ndoa, lakini kadiri umri unavyoongezeka yanatokea mabadiliko ambayo yanaweza kuleta matatizo usiyotarajia.

Hata hivyo wazee wana mahitaji sawa ya raha na ustawi kama watoto, vijana, na watu wazima, na ingawa mienendo yao haiangaziwi vilivyo katika jamii hasa linapokuja suala la kujamiana.

Kuendelea kufanya mapenzi wakati wa mchakato wa kuzeeka kunapaswa kuchukuliwa kuwa haki ya msingi na kiashiria muhimu cha ubora wa maisha.

Claudia na Luis walikutana wakiwa vijana. Walipendana sana na kila mmoja alikuwa akimuwaza mwenzake walipokuwa mbali mbali na walipokutana miili yao ikasisimka kwa kusuguana tu. Walifurahia kufanya mapenzi mara kwa mara.

Image: GETTY IMAGES

Jinsi ya kuimarisha uhusiano wa kingono uzeeni

Kwa baadhi ya wanawake, kukomaa kwa hedhi humaanisha mwisho wa shughuli za ngono katika ndoa. Akina mama wengine huwa na hamu sana ya ngono kwa sababu hawana hofu ya kushika mimba. Hata hivyo, wanawake wote wanahitaji upendo. Hakuna ushuhuda wa kuonyesha kuwa, kwa sababu ya umri, mwanamke hawezi kufurahia ngono.

Baadhi ya mabadiliko katika mwili wa mwanamke humzuia kushiriki ngono:

  • Wanawake huenda wakapoyeza hamu ya kushiriki ngono (wanaume pia huathirika).
  • Sehemu ya uzazi hukauka, na hii hufanya tendo la ngono kutofurahisha, au kumfanya mwanamke akapata maambukizi kwenye sehemu hii au katika njia ya kupitisha mkojo, kwa urahisi.

Umri wa Uzee

Je ni umri wa uzee ambao mtu anaanza kushindwa kufanya tendo la ndoa ni upi?

Kwa mujibu wa utafiti, umri wa uzee ambao mwanaume na mwanamke huenda wakapata matatizo haya ni kuanzia miaka sitini endapo walikuwa na afya nzuri tangu walipokuwa vijana.

Hata hivyo wanawake na wanaume wanaweza kupata mabadiliko na matatizo katika tendo la ndoa hata wakiwa ujanani au kabla ya umri wa miaka sitini endapo uwatakuwa na matatizo mbalimbali ya kiafya.

Utafiti mwingine pia unaonyesha kuwa idadi kubwa ya matatizo haya hutokea katika umri wa miaka 35 hadi 55, miongoni mwa wanaume na wanawake kutokana na sababu mbalimbali.