•Wadau kadhaa kutoka Dubai kwa sasa wanahudhuria hafla ya Idara ya Uchumi na Utalii ya Dubai katika hoteli ya MovenPick jijini Nairobi.
Wadau kadhaa kutoka Dubai kwa sasa wanahudhuria hafla ya Idara ya Uchumi na Utalii ya Dubai katika hoteli ya MovenPick jijini Nairobi.
Meneja wa Kanda Stela alisema kuwa wadau hao wapo nchini kwa ajili ya kuonyesha ofa walizonazo kwa wasafiri wa Afrika Mashariki.
Hafla hiyo kawaida hufanyika kila mwaka kwa miaka mitano iliyopita.
"Kwa sababu ya janga la Covid-19, tulilazimika kuchukua mapumziko mwaka wa 2020 na kupanga upya," meneja wa konda alisema.
Siku ya leo, Alhamisi, washiriki watakuwa na nafasi ya kushiriki katika mchezo wa bahati nasibu wa Dubai.
Zawadi hizo ni pamoja na safari iliyolipiwa kikamilifu ya kwenda Dubai.