Mfanyibiashara hakumuambia mkewe siri ya kutokuwa na uwezo 'kurusha risasi', alihamakishwa na ujauzito wake

Shida moja iliyokuwepo ni kuwa Jonathan Mukundi, 42, hakutaka watoto ila mkewe Philomena Njeri, 30, alikuwa na hamu ya kuwa na familia

Muhtasari

•Imefichuka kuwa Mukundi hakuwahi fahamisha mkewe kuwa hakuwa na nguvu za kuzalisha. Wawili hao hata walijaribu uzazi wa Kisayansi (IVF) ila mume alifahamu vizuri kuwa juhudi zile zilikuwa bure tu.

•Utata uliibuka wakati Njeri alipata ujauzito na hapo mumewe akajua kuwa alikuwa akisakata densi nje.

•Polisi walipata miili ya wawili hao ndani ya chumba chao cha kulala baada ya rafiki wao wa karibu kuwafahamisha kuwa Mukundi hakuwa anashika simu zake, jambo ambalo si la kawaida.

Jonathan Mukundi na bibiye Philomena Njeri
Jonathan Mukundi na bibiye Philomena Njeri
Image: HISANI

Wanandoa wawili waliopatikana wakiwa wamefariki ndani ya nyumba yao maeneo ya Kirigiti Kiambu walikuwa wamefunga ndoa kwa miaka mitano na maisha yao kwenye ndoa yalionekana kuwa sawa.

Shida moja iliyokuwepo ni kuwa Jonathan Mukundi, 42, hakutaka watoto ila mkewe Philomena Njeri, 30, alikuwa na hamu ya kuwa na familia.

Imefichuka kuwa Mukundi hakuwahi fahamisha mkewe kuwa hakuwa na nguvu za kuzalisha. Wawili hao hata walijaribu uzazi wa Kisayansi (IVF) ila mume alifahamu vizuri kuwa juhudi zile zilikuwa bure tu.

Utata uliibuka wakati Njeri alipata ujauzito na hapo mumewe akajua kuwa alikuwa akisakata densi nje.

Majirani na marafiki walipigwa na butwaa siku ya Jumanne wakati polisi walipata miili ya wawili hao ambao walikuwa wamefunga ndoa kwa miaka 6.

Marafiki wa karibu na wafanyakazi nyumbani kwao Kirigiti wamesema kuwa raha katika boma ile ilianza kudidimia haraka katika mwaka wa sita wa ndoa.

Baadhi ya waliojuana na wawili hao walitoa hisia tofauti kuhusu hali yao. Mtu mmoja aliyefahamu wawili hao aliambia Star kuwa Mukundi hakutaka watoto kwani tayari alikuwa na wawili kutoka ndoa yake ya hapo awali. Mwingine alisema kuwa Mukundi alikuwa ameambia rafiki wa karibu kuwa hakuwa na uwezo wa kuzalisha.

Rafiki wa karibu alithibitisha kuwa Mukundi alikuwa na watoto wawili na mke aliyekuwa Ubelgiji na kusema kuwa Njeri alikuwa na ujauzito ambao alipata kupitia IVF.

Rafiki huyo ambaye hakuta kutajwa alisema kuwa mzozo ulianza wakati Mukundi aligundua kuwa Njeri alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa wafanyakazi katika duka lao la kuuza vipuri.

Jirani mwingine ambaye hakutaka kutajwa pia alisema kuwa Mukundi alikasirika baada ya kugundua kuwa mkewe alikuwa mjamzito na hakuwahi mfahamisha kuwa hana uwezo wa kuzalisha.

"Alikuwa na hasira hata akatishia kumuangamiza au kujiangamiza mwenyewe" Jirani huyo alisema.

Polisi walipata miili ya wawili hao ndani ya chumba chao cha kulala baada ya rafiki wao wa karibu kuwafahamisha kuwa Mukundi hakuwa anashika simu zake, jambo ambalo si la kawaida.

Kulingana na ripoti ya polisi, Mukundi ambaye ni mmiliki wa bunduki kihalali alimpiga mkewe risasi tatu  kabla ya kujitoa uhai kwa kujipiga risasi kichwani.

Bastola ya mwanabiashara huyo ilipatikana katika eneo la tukio.

Kwa mengi tembelea  https://www.the-star.co.ke/

(Utafsiri: Samuel Maina)