Kijakazi asimulia jinsi kuchelewa kufikisha nywele bandia kulifanya afutwe kazi na mtangazaji mashuhuri

Obunga amesema kuwa kazi ya ujakazi ni kama utumwa na wengi wao hupitia wakati mgumu kwa nyumba za waajiri wao.

Muhtasari

•Marion Obunga (33) kama anavyojitambulisha kwenye mtandao wa Twitter amesema kuwa amekuwa afanya kazi ya ujakazi kwa kipindi  cha miaka 7 na amepitia changamoto chungu nzima.

•Obunga amesema kuwa mtangazaji huyo ambaye hajatambulishwa hakuwa akimlipa kwa wakati wala kumpa siku za kupumzika na alimlazimisha kuzungumza kwa kiingereza kila wakat

Image: TWITTER// MARION OBUNGA

Mwanamke mmoja amewaacha wanamitandao wakiwa na butwaa baada ya kufunguka kuhusu maisha magumu amepitia akihudumu kama kijakazi.

Marion Obunga (33) kama anavyojitambulisha kwenye mtandao wa Twitter amesema kuwa amekuwa afanya kazi ya ujakazi kwa kipindi  cha miaka 7 na amepitia changamoto chungu nzima.

Tukio moja alilosimulia ambalo limeibua mdahalo mkubwa kwenye mtandao wa Twitter amesema kuwa alipitia 'Jahanamu' akimfanyia kazi mtangazaji mmoja wa runinga mashuhuri nchini.

Obunga amesema kuwa mtangazaji huyo ambaye hajatambulishwa hakuwa akimlipa kwa wakati wala kumpa siku za kupumzika na alimlazimisha kuzungumza kwa kiingereza kila wakati.

"Malipo ilikuwa shida, sikuwa na siku za kupumzika, sikuruhusiwa kuzungumza naye ana kwa ana na nililazimishwa kuongea kiingereza kila wakati. Alikuwa akishinda kwa blogu na kukabiliwa na kashfa tele" Obunga aliandika.

Mwanamke huyo amesimulia tukio ambalo lilisababisha kufutwa kazi kwake akisema kuwa hata hakupokea malipo yoyote.

"Kuna wakati alikuwa na hafla maeneo ya Westlands na akiambia nimpelekee 'wig'(nywele bandia) fulani kwa dharura. Kulikuwa na msongamano mkwubwa wa magari na nilikuwa ndani ya Uber. Nikachelewa kufika na wakati nilifika akachukua 'wig'(nywele bandia) hiyo, akanitupia kwa uso na kunizaba kofi na kunifuta kazi papo hapo. Sikuwai lipwa mshahara." Obunga alisimulia.

Obunga amesema kuwa kazi ya ujakazi ni kama utumwa na wengi wao hupitia wakati mgumu kwa nyumba za waajiri wao.

"Tunaishi kwa nyumba za watu na kuwa watumwa. Na pia mshahara ni kama matusi ila tunaendelea kujikaza" Alisema Obunga.