Mshangao baada ya mwanadada kutishia kuchapisha orodha ya 'mafisi' ambao ameambukiza UKIMWI

Wanamitandao wengi wamekita kambi kwenye ukurasa wake wa Facebook wakisubiri kusoma orodha hiyo wakati itakapotolewa.

Muhtasari

•Ruth James kama anavyojitambulisha kwenye mtandao wa Facebook ametoa ilani kwa wanaume zaidi ya 500 ambao anadai kuwa ameshiriki  tendo la ndoa nao.

•Mwanadada huyo anadai kuwa ameumia sana na kwa sasa anaona suluhu ya kipekee iliopo ni kufa.

Mwanamke mmoja amewashangaza Wakenya baada yake kutishia kutoa orodha ya wanaume ambao amelala nao na kuwaambukiza virusi vya UKIMWI nchini.

Ruth James kama anavyojitambulisha kwenye mtandao wa Facebook ametoa ilani kwa wanaume zaidi ya 500 ambao anadai kuwa ameshiriki  tendo la ndoa nao.

Kwenye ukurasa wake wa Facebook ambao una wafuasi zaidi ya 50,000 Ruth amekuwa akiandika jumbe za kutatanisha akitishia kufichua majina na sura za wote ambao wamewahi kumnyemelea.

"Nataka kufichua kila mtu ambaye nimeambukiza na UKIMWI" ujumbe mmoja wa Ruth ulisoma.

Mwanamke huyo anadai  kuwa kunao  'mafisi' zaidi ya mia moja mtandaoni  Facebook ambao wanahofia kutajwa

"Unanichezea. Wanaume 100 wa Facebook wanataka kufa stress" Ruth aliandika kwa lugha ya dholuo kwenye ujumbe wake mmoja.

Mwanadada huyo anadai kuwa ameumia sana na kwa sasa anaona suluhu ya kipekee iliopo ni kufa.

"Kufa ndicho kitu kizuri zaidi. Nimeumia sana." Ruth aliandika.

Wanamitandao wengi wamekita kambi kwenye ukurasa wake wa Facebook wakisubiri kusoma orodha hiyo wakati itakapotolewa.

Kunao baadhi ya wanamitandao ambao wametia juhudi kutafuta picha ambazo mwanadada huyo amepigwa na wanaume tofauti wakidai kuwa hao ni baadhi ya wahasiriwa wake. 

Hata hivyo Radio Jambo imebainisha kuwa bado orodha rasmi haijachapishwa.