DCI wamkamata jamaa aliyemuua mpenzi wake Kerugoya

Muhtasari
  • Wapelelezi wa DCI wamemkamata mwanamume mmoja huko Kerugoya, kaunti ya Kirinyaga, kwa mauaji ya mpenzi wake Jumanne jioni
Pingu
Image: Radio Jambo

Wapelelezi wa DCI wamemkamata mwanamume mmoja huko Kerugoya, kaunti ya Kirinyaga, kwa mauaji ya mpenzi wake Jumanne jioni.

Kennedy Nyamu alikamatwa na wapelelezi wa Kirinyaga Jumanne usiku, baada ya kumshambulia vikali Edith Muthoni, mwenye umri wa miaka 27.

Kulingana na meneja wa Hospitali ya Rufaa ya Kerugoya, Norman Gitari, marehemu alifikishwa hospitalini akiwa katika hali mbaya, na msamaria mwema.

"Wafanyakazi wake walijaribu kuokoa maisha yake, na kusababisha msimamizi wa hospitali kuwajulisha maafisa wetu walio katika kituo cha polisi cha Kerugoya," DCI alisema.

DCI iliongeza kuwa uchunguzi ulianzishwa mara moja na kusababisha kukamatwa kwa mpenzi wa marehemu kama mshukiwa muhimu wa mauaji hayo.

"Mshukiwa huyo aliongoza wapelelezi hadi eneo la mauaji katika kijiji cha Kianjege, ambapo walitumia muda wao wa usiku kuchunguza zaidi eneo la tukio kwa dalili zaidi za uhalifu huo mbaya," DCI aliendelea kusema.

Mshukiwa huyo yuko katika mikononi mwa polisi, akisubiri kufikishwa mahakamani kujibu mashataka hayo ya mauaji.