Nikishindwa na kazi kwa miaka 5 mtafute mtu mwingine-Ruto awaambia wakazi wa Nyeri

Muhtasari
  • Naibu Rais William Ruto amesema sasa ana nia ya kuhudumu kwa miaka 5 pekee, wala sio kumi
Naibu rais William Ruto akifanya kampeini
Naibu rais William Ruto akifanya kampeini
Image: MAKTABA

Naibu Rais William Ruto amesema sasa ana nia ya kuhudumu kwa miaka 5 pekee, wala sio kumi.

Huku akirejea matamshi ya Rais Uhuru Kenyatta, ambaye awali alisema atahudumu kwa miaka 10 na kumkabidhi kuhudumu pia kwa miaka 10, Ruto alitoa wito kwa Wakenya kumpa muhula mmoja.

Alisema baada ya miaka mitano, Wakenya wataamua iwapo watamwongezea miaka mitano ya ziada au watafute mtu mwingine kulingana na utendakazi wake.

"Tumekua na mjadala ambayo rais wetu alituambia yake kumi na yangu kumi. Lakini mimi sitaki kumi, nataka tuandikane hii ya miaka tano kwanza. Nikifaulu kufanya kazi kwa hii miaka tano mniongeze ingine. Nikishindwa mtafute mtu mwingine," Alizungumza Ruto.