Msafiri akamatwa uwanja wa ndege JKIA na pesa za kigeni 238M taslimu

Muhtasari

• Msafiri amekamatwa na maafisa kutoka mamlaka ya utozaji ushuru katika uwanja wa kimataifa wa JKIA akiwa na fedha za kigeni zenye thamani ya milioni 238 za Kenya, zikiwa taslimu.

TWITTER
Image: DCI

Msafiri amekamatwa na maafisa kutoka mamlaka ya utozaji ushuru katika uwanja wa kimataifa wa JKIA akiwa na fedha za kigeni zenye thamani ya milioni 238 za Kenya, zikiwa taslimu.

Msafiri huyo mwenye urai wa Kenya aliwaziri uwanjani humo akitokea Bujumbura, Burundi na baada ya uchunguzi wa mizigo aliyokuwa nayo, pesa hizo zikapatikana naye ambapo alitoa hati za kuzisafirisha zikiwa  tofauti, kupelekea kuzuiliwa kwake kwa uchunguzi Zaidi.

Msafiri huyo aliwasilisha hati kwamba pesa hizo zilikuwa zinatoka Banque de Credit de Bujumbura (BCB) na kusema kwamba alikuwa anazipokeza kwa kampuni ya Brinks Global Services, Kenya ambapo alipewa kibali cha kuondoka na kitengo cha utoaji kibali, Clearance Unit ili kuzipeleka kwenye kampuni hiyo.

Hapo ndipo alitoka na kuingia na fedha hizo kwa kibanda cha Swissport Cargo akiwa na hati ya kuzisafirisha, akiwa na lenga la kuzisafirisha kuenda kampuni ya Global Services, iliyoko Uingereza.

Jambo hili lilizua mkanganyiko kwani maafisa hao walibaini kwamba hati hizo zilikuwa zinatofautiana na hati alizozionesha akiingia na hapo maafisa wa mamlaka ya ukusanyaji ushuru ikaingilia kati na kumshikilia.

KRA Imeitaka mamlaka ya kurejesha mali ya umma kuingilia kati na kusaidia katika uchunguzi Zaidi wa kisa hicho ambacho kimetajwa kuwa na uswahiba wa ulaghai wa pesa almaarufu ‘wash wash’

Msafiri huyo mwenye urai wa Kenya aliwaziri uwanjani humo akitokea Bujumbura, Burundi na baada ya uchunguzi wa mizigo aliyokuwa nayo, pesa hizo zikapatikana naye ambapo alishindwa zinakoelekea kwa kuonesha risiti tofauti, kupelekea kuzuiliwa kwake kwa uchunguzi Zaidi.

Mwanaume huyo aliwasilisha tamko kwa njia ya maandishi kwamba pesa hizo zilikuwa zinatoka Banque de Credit de Bujumbura (BCB) na kusemac kwamba alikuwa anazipokeza kwa kampuni ya Brinks Global Services, Kenya ambapo aliapewa kibali cha kuondoka na kitengo cha utoaji kibali, Clearance Unit ili kuzipeleka kwenye kampuni hiyo.

Hapo ndipo aliziwasilisha fedha hizo kwa kibanda cha Swissport Cargo akiwa na hati ya kuzisafirisha, akiwa na lenga la kuzisafirisha kuenda kampuni ya Global Services, iliyoko Uingereza.

Jambo hili lilizua mkanganyiko kwani maafisa hao walibaini kwamba hati hizo zilikuwa zinatofautiana na hati alizozionesha akiingia na hapo maafisa wa mamlaka ya ukusanyaji ushuru ikaingilia kati na kumshikilia.

KRA Imeitaka mamlaka ya kurejesha mali ya umma kuingilia kati na kusaidia katika uchunguzi Zaidi wa kisa hicho ambacho kimetajwa kuwa na uswahiba wa ulaghai wa pesa almaarufu ‘wash wash’