DP Gachagua aahidi kumsomesha msichana kipofu hadi amalize masomo

Msichana huyo mwenye ulemavuu wa macho aliimba wimbo kwa sauti iliyomfurahisa naibu wa rais huko Kisumu.

Muhtasari

• Jane, alikuwa miongoni mwa wanafunzi waliotumbuiza katika hafla ya miziki ya shule nchini Kenya huko Kisumu.

• Msichana huyo anasoma shule ya walemavu wa macho ya Thika.

Gachagua asema atafadhili masomo ya msichana kipofu
Gachagua asema atafadhili masomo ya msichana kipofu
Image: Twitter

Naibu wa rais Rigathi Gachagua amefurahisha mioyo ya wengi baada ya kusema kwamba amejitolea kusimamia elimu ya mwanafunzi mmoja mwenye ulemavu wa macho – Kipofu.

Rigathi Gachagua alisema haya katika hafla ya muziki ya shule inayoendelea katika kaunti ya Kisumu ambapo pamoja na viongozi wengine waliudhuria hafla hiyo Ijumaa.

Mwanafunzi huyo wa kike kwa jina Jane kutoka shule ya vipofu ya Thika aliimba wimbo katika hafla hiyo, kitu ambacho kilimnfurahisha mno Gachagua na kuweka wazi kwamba kuanzia alipofikia kimasomo, sasa itakuwa zamu yake kumsomesha mpaka atakapofika kilele cha masomo yake.

Gachagua alisema msichana huyo alikuwa amemvutia kwa sauti yake tamu yenye mirindimo ya aina yake mithili ya ninga.Naibu huyo wa rais alishangaa kwamba ilikuwa sauti tamu zaidi ambayo hakuwahi kuisikia kwa kipindi cha muda mrefu maishani mwake.

“Nimemsikiliza mwanafunzi wa Kidato cha Nne kutoka Shule ya Thika ya Walemavu wa Macho kwa jina June. Nimesikia moja ya sauti tamu sana ambayo simewahi kusikia maishani mwangu. Kwa kutambua wimbo huo na kumtia moyo msichana huyo mdogo, nitasimamia elimu yake hadi aendako," alisema huku kukiwa na shangwe tele kutoka kwa umati.

Gachagua pia alifurahisha wengi alipotimba jukwaani na ala ya muziki ya kamba nane kucheza muziki huku watu kadhaa waliokuwemo wakimsherehekea kwa mbwembwe.Vile vile, alitambua jina la kimajazi ambalo amepandikwa hivi majuzi la Riggy G na kusema ni kuonesha jinsi vijana wadogo wanavyomiliki sifa ya kubuni vitu na majina.

Gachagua alisema wala haoni kama jina hilo ni baya na kulikiubali mia kwa mia.